Kimwakaleli
JF-Expert Member
- Apr 16, 2018
- 7,755
- 11,737
Biblia haimlaumu mtu kwa sababu ni tajiri;Wala haisemi kuwa utajiri ni chimbuko la uovu wote.Badala yake maandiko yanasimama kuwa Mungu atoaye uwezo wa kupata utajiri Na uwezo huu na talanta iliyo nzuri kama ikitolewa kwa Mungu na kutumia na kuendesha kazi yake .Biblia haimlaumu uwezo wa ubongo au ubingwa; Maana hivi hutokana na Hekima itolewayo na Mungu.Hatuwezi kufanya moyo kuwa Safi na mtakatifu kwa kuuvika magunia au kuzinyima kaya vitu vyote vinvyoleta faraja, chakula kizuri au Hali Nzuri.
Maandiko matakatifu yanatufundisha kuwa Mali ni hatari inaposhindanishwa na hazina ya kutokuharibika.Mali inakuwa mtego tu wakati inapotoa mawazo yote kutoka kwa mambo yote ambayo Mungu anataka atendewe.Wale wanaobadilisha mambo ya utukufu wa milele na mambo madogo ya urembo wa Dunia,wanaobadilisha makao ya milele na Maisha ya miaka micha he,nao wanafanya u haguzi usio wa hekima.Hivyo ndivyo Esau aliyobadilisha haki ya uzaliwa wake wa Kwanza na chakula;na Balaamu alipokataa mapenzi ya Mungu ili apate zawadi ya Mfalme wa Midiani na Yuda naye alipimsaliti Bwana wa utukufu kwa vipande thelasini vya Fedha.
Ni kupenda fedha ambako Neno la Mungu linalaumu kuwa shina la uovu.Fedha yenyewe ni karama kwa binadamu ili utumiwe kwa uaminifu katika kazi yake.Mungu alimbariki Ibrahimu na akamtajirisha kwa mifugo,fedha na dhahabu.Na Biblia inasema kuwa hii ni dalili ya kufadhiliwa na Mungu,kwani Mungu aliwapa Daudi,Sulemani,Yehoshafati na Hezekia utajiri mwingi na Heshima.
Kama zilivyo karama zingine za Mungu,kuwa na Mali huongeza wajibu mwingi na majaribu yake ya pekee.Ni wangapi ambao katika dhiki wangeludumu kuwa waaminifu kwa Mungu,lakini wameanguka katika kivutio chenye ushawishi Cha utajiri.Pamoja na kumiliki utajiri, Tamaa itawalayo ya ubinafsi wa asili hufunuliwa.Ulimwengu umelaaniwa Leo na uchoyo na kujipenda nafasi kwa wake wanaoabudu Mali
.
R&H.Mei 16,1882.(R&H_Review and Herald).