Kwa benki za hapa Bongo kama hufanyi kazi sio rahisi kusikilizwa achia mbali kupewa mkopo. Kuna baadhi ya benki siku hizi hati za nyumba za kawaida wanagoma,labda kama ni nyumba ya biashara wanakubali. Kwa hiyo dhamana ni lazima.Kama una dhamana ya kuaminika nenda Twiga Bancorp pale, wale riba yao nafuu kidogo. Kama ni mwajiriwa basi ndani ya siku saba kitu tayari, ili mradi mwajiri wako awe tayari kukupa support kwanza kwa kupitishia mshahara wako kwao.
Vinginevyo, ukiwa na sifa hizo jaribu akiba commercial bank wako vizuri pia.