Kupata mimba baada ya kujifungua

Kupata mimba baada ya kujifungua

Ok9

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
4,549
Reaction score
4,133
Wakuu mwanamke anaweza kupata mimba muda gan baada ya kujifungua ikiwa haoni siku zake?

Kuna uwezekano wa kupata mimba ukiwa hujaingia kwenye siku zako?
 
wakuu mwanamke anaweza kupata mimba muda gan baada ya kujifungua ikiwa haoni siku zake...?...
.
.
.

2.
kuna uwezekano wa kupata mimba ukiwa hujaingia kwenye siku zako....?

hawezi kupata mimba ikiwa haoni siku zake.kipindi.cha kupata mimba baada ya kujifungua hutofautiana mtu na mtu kulingana na muda anaonyonyesha.kama ananyonyesha mara kumi na kuendelea kwa siku anaweza kukaa hata miaka 2 bila kupata mimba.kama ujuavyo kunyonyesha pia ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango zile hormons ambazo zinatakiwa kurutubisha mayai basi zinakua zipo busy kuzalisha maziwa so kwa kipindi hiki basi mama hawez kuona siku zake.mwingine anaweza kujifungua then after one month akaanza kuona siku zake.point ni kwamba kama haoni siku zake hawez kubeba mimba.
 
nashkuru sana nimekuelewa vizuri...
 
ameline, chaka hilo aisee. Ukisikia kuumbuka na voda fasta ndio hiyo. Mwanamke baada ya kujifungua anaweza kupata mimba kabla ya kuanza kuona siku zake. Huyo ambae mtoa mada anamuongelea sio ajabu anayo mimba tayari.

Mtoa mada, hayo mambo unapaswa kuongea na daktari wako ama wenu kabla hata ya kujifungua. Siku salama ni zile 40 za mwanzo tu. Siku unarudi kwa dr na kulalama hujaona siku anaweza kukusapraizi na ujumbe kuwa una mimba ya miezi mitatu.
 
Last edited by a moderator:

imepimwa lkn........hakuna
 
inawezekana vipi mimba ikatungwa pasi na kuwepo urutubishwaji wa yai? hamnaga hiyo ndugu.wapo watu wanalia usiku na.mchana wapate siku zao ili wabebe mimba labda ushee hako ka uzoefu ka kupatikana na mimba pasi na kupata bleed tafadhali
 
nakubaliana na King'asti. kuna uwezekano kupata mimba kabla ya kuona siku zako baada ya kujifungua. principle ni kwamba, ili upate siku zako lazima upevue yai ila lisirutubishwe. kama unanyonyesha unakuwa mara nyingi unalindwa na phenomenon tunaita "lactational amenorrhea" , kwamba mfumo wako wa uzazi unazuiwa kuivisha na kupevusha mayai,, hivyo hupati siku zako. na si kweli kwamba zile hormone za kupevusha mayai zitakuwa zime-concentrate kwenye kutengeneza maziwa,, tuheshimiane tafadhali . hormine hizi ni tofauti na hu-interact only through negative feedback kuleta hyo lactation amenorrhea.

kwa hvyo basi, kuna uwezekano kwamba ukapevusha yai na likarutubishwa, hivyo ukabeba mimba nyingine bila ya kurudi kwenye siku zako za bleed. hii ni rare kwa wale wanaonyonyesha vizuri (kama nilivyoeleza juu) , lakini uwezekano bado upo.
 
mmm kumbe hazina formular
 
Kutokwa damu inahusiana na hormones na kujengwa kwa ukuta ambao unaandaa mazingira ya kushikiza mimba kwenye kizazi. Kupevuka yai nayo ni process tofauti. Kurutubishwa kwa yai ndio inahusiana na uwepo wa mbegu za mwanaume.

Kwa hiyo unaweza ukakutana na mumeo na mimba ikatungwa hata kama mzunguko wako haujaanza rasmi. Kutegemeana na hormones, wanawake tofauti wanakuwa na upevushaji mayai kwa siku tofauti hata kama mzunguko wao wa damu ni siku 28 tu. Kuna mwingine anaweza kutunga mimba siku ya 25, na bado mzunguko ni siku 28.

Bottom line, ukiwa na shida na maswali yoyote ya afya ni muhimu sana kujadiliana na daktari mhusika. Kuna mengi sana ya kujifunza kila siku
inawezekana vipi mimba ikatungwa pasi na kuwepo urutubishwaji wa yai? hamnaga hiyo ndugu.wapo watu wanalia usiku na.mchana wapate siku zao ili wabebe mimba labda ushee hako ka uzoefu ka kupatikana na mimba pasi na kupata bleed tafadhali
 
Tunajifunza kila siku.
Na kwa sababu kuna uwezekano wa kutunga mimba hata kabla ya kuona siku baada ya kujifungua, inashauriwa kutotumia njia zozote za uzazi wa mpango hadi mama ananapata siku zake. Na ni muhimu kupata huduma hiyo ndani ya siku 10 toka aanze siku zake.
ameline, kuna kilio kingine tofauti. Unaenda kwa dr unamuambia nimemaliza maternity, nimeanza na kazi ila bado sijaanza kuona siku zangu. Unapewa 'good news' umeshatinga mimba ya miezi miwili. Lazma akili ihame kwa mvua ya baraka lol

king'asti nashukuru kwa ushauri wako looh! sikulijua hili ila nililizungumzia kama nilivyoambiwa na doctor na nimepractice wala sijashika mimba
 
wakuu mwanamke anaweza kupata mimba muda gan baada ya kujifungua ikiwa haoni siku zake...?...
.
.
.

2.
kuna uwezekano wa kupata mimba ukiwa hujaingia kwenye siku zako....?

hebu ingia hapa ilishajadiliwa humu upate mwanga zaidi
jamiiforums.com/jf-doctor/664390-kutopata-hedhi-kwa-muda-mrefu-baada-ya-kujifungua.html
 
King'asti unatumia nguvu kubwa sana kumuelimisha ameline lkn njia nyepesi mwambie hivi kwani ili damu ya hedhi itoke si utanguliwa na yai kupevuka? kama ndio anafikiri haiwezeanaa yai hili likarutubiushwa kabla hata ya kuona siku?
Ukuta hujengwa na separate process na ukuta huu hu -erode baada ya yai kufariki.
Kutokwa damu inahusiana na hormones na kujengwa kwa ukuta ambao unaandaa mazingira ya kushikiza mimba kwenye kizazi. Kupevuka yai nayo ni process tofauti. Kurutubishwa kwa yai ndio inahusiana na uwepo wa mbegu za mwanaume.

Kwa hiyo unaweza ukakutana na mumeo na mimba ikatungwa hata kama mzunguko wako haujaanza rasmi. Kutegemeana na hormones, wanawake tofauti wanakuwa na upevushaji mayai kwa siku tofauti hata kama mzunguko wao wa damu ni siku 28 tu. Kuna mwingine anaweza kutunga mimba siku ya 25, na bado mzunguko ni siku 28.

Bottom line, ukiwa na shida na maswali yoyote ya afya ni muhimu sana kujadiliana na daktari mhusika. Kuna mengi sana ya kujifunza kila siku
 
Last edited by a moderator:
Tunajifunza kila siku.
Na kwa sababu kuna uwezekano wa kutunga mimba hata kabla ya kuona siku baada ya kujifungua, inashauriwa kutotumia njia zozote za uzazi wa mpango hadi mama ananapata siku zake. Na ni muhimu kupata huduma hiyo ndani ya siku 10 toka aanze siku zake.
ameline, kuna kilio kingine tofauti. Unaenda kwa dr unamuambia nimemaliza maternity, nimeanza na kazi ila bado sijaanza kuona siku zangu. Unapewa 'good news' umeshatinga mimba ya miezi miwili. Lazma akili ihame kwa mvua ya baraka lol

was once suprised wit the same scenario.......
Ilibidi niache kazi nikakaa ndani hadi nikajifungua. Kwasasa wanaitwa mapacha wa nje.
Its not safe ku assume sitoconceive baada ya kujifungua kisa sijaona period nope, af ilivyo kuwa ujinga kwasabb hujaanza kupata period utaassume kwamba ni kawaida nanyonyesha kumbe kijusi kinakua tumboni tayari.
 
dada angu alipatamimba kabla hata ya arobain ya mwanae mchanga
 
hawezi kupata mimba ikiwa haoni siku zake.kipindi.cha kupata mimba baada ya kujifungua hutofautiana mtu na mtu kulingana na muda anaonyonyesha.kama ananyonyesha mara kumi na kuendelea kwa siku anaweza kukaa hata miaka 2 bila kupata mimba.kama ujuavyo kunyonyesha pia ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango zile hormons ambazo zinatakiwa kurutubisha mayai basi zinakua zipo busy kuzalisha maziwa so kwa kipindi hiki basi mama hawez kuona siku zake.mwingine anaweza kujifungua then after one month akaanza kuona siku zake.point ni kwamba kama haoni siku zake hawez kubeba mimba.

Naomba nitofautiane na wewe,baada ya kujifungua,ni dhahiri kwamba njia ya uzazi ya mwanamke inakua wazi na ni kipindi ambacho mwanamke anaweza kubeba mimba kwa urahisi zaidi kuliko wakati wowote bila kujali ameona siku zake au haoni siku zake,na kuhusu hedhi inategemea na mtu binafsi sina uhakika kama kuna uhusiano kati ya kunyinyesha na kupata hedhi( I stand to be corrected) mimi niliana kupata mzunguko wa hedhi mwezi mmoja baada ya kujifungua na nilikua nanyonyesha zaidi ya mara kumi.

Cc MziziMkavu,
 
Last edited by a moderator:
Kutokwa damu inahusiana na hormones na kujengwa kwa ukuta ambao unaandaa mazingira ya kushikiza mimba kwenye kizazi. Kupevuka yai nayo ni process tofauti. Kurutubishwa kwa yai ndio inahusiana na uwepo wa mbegu za mwanaume.

Kwa hiyo unaweza ukakutana na mumeo na mimba ikatungwa hata kama mzunguko wako haujaanza rasmi. Kutegemeana na hormones, wanawake tofauti wanakuwa na upevushaji mayai kwa siku tofauti hata kama mzunguko wao wa damu ni siku 28 tu. Kuna mwingine anaweza kutunga mimba siku ya 25, na bado mzunguko ni siku 28.

Bottom line, ukiwa na shida na maswali yoyote ya afya ni muhimu sana kujadiliana na daktari mhusika. Kuna mengi sana ya kujifunza kila siku

Ujauzito kama huu
[h=1]Royal baby: Prince William and Kate expecting second child[/h]Sio ajabu umetungwa ndani ya miezi michache baada ya kujifungua
 
Mimba inapatikana kabla ya kuingia kwenye siku,
binafsi niliona siku baada ya siku 30 toka kujifungua,hivyo ningecheza hapo katikati ningeweza kupata mimba.

Back
Top Bottom