- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimekuwa katika jamii ambayo unaambiwa ni kawaida mwanamke kupata maumivu anapokuwa katika hedhi, kuna baadhi ya wanawake wamekuwa wakipata maumivu makali wakati wakuingia hedhi na kutokwa na damu nyingi na hadi kupitiliza siku 7 je shida ni nini na suluhisho ni kuzaa mapema?
- Tunachokijua
- Maumivu wakati wa hedhi kitaalamu hujulikana kama Dysmenorrhea (Menstrual Cramps), kwa mujibu wa Andiko lilochapishwa katika tovuti ya Cleverland Clinic ya nchini Marekani, ni maumivu ambayo mwanamke huyapata kipindi cha hedhi na huanza siku chache kabla ya hedhi na kupungua siku chache baada ya hedhi kulingana na mtu husika.
Maumivu wakati wa hedhi (Dysmenorrhea) yamegawanyika katika aina mbili ambapo aina ya kwanza ni maumivu ya hedhi ya kawaida haya ni maumivu yasiyo na sababu maalum katika kipindi cha hedhi, na aina ya pili ni maumivu ya hedhi yanayotokana na hali kama vile endometriosis ambapo Kwa mujibu wa tovuti ya medicover hospitals ni hali ambayo tishu zinazofanana na endometriamu hukua nje ya uterasi, mara nyingi kwenye ovari, mirija ya uzazi, au sehemu ya nje ya uterasi. Tishu hii huongezeka, kuchanika, na hutoka damu kwa kila mzunguko wa hedhi.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini nini?
JamiiCheck imepitia machapisho mbalimbali ikiwepo chapisho lililochapishwa na kituo binafsi cha taaluma cha tiba kilichopo nchini marekani kinachojulikana kama Mayo Clinic ambacho kinaeleza kuwa aina ya kawaida ya maumivu ya hedhi (primary Dysmenorrhea) huweza kupungua na kupata nafuu kadri umri unavyozidi kuongezeka na wakati mwingine baada ya kujifungua hivyo kuonesha uwezekano wa kupungua kwa maumivu makali ya hedhi baada ya kupata mtoto.
Kadhalika chapisho kutoka tovuti ya Cleverland Clinic linathibitisha uwepo wa uwezekano wa kupungua kwa maumivu ya hedhi baada ya kupata mtoto lakini pia kadri umri unavyozidi kuongezeka inaweza kuwa chanzo cha kupunguza maumivu.
Kwa mujibu wa tafiti, mabadiliko ya homoni za Norepinephrine baada ya kujifungua huathiri mijongeo ya misuli ya mji wa uzazi, hivyo kupunguza maumivu ya hedhi kwa baadhi ya wanawake. Chapisho lingine linalothibitisha jambo hili linapatikana hapa
Inashauriwa kumuona mtaalamu wa afya mara baada ya kupata kupata maumivu wakati wa hedhi ili kufanya vipimo sahihi kwa muhusika ili kuweza kutambua chanzo cha maumivu hayo ambapo hupatiwa matibabu maalumu kutokana na chanzo cha maumivu wakati wa hedhi.