Ili ufanikishe wazo lako kuna mambo ambayo ni ya msingi inabidi uyazingatie (hasa unapohitaji lipatiwe ufadhili).
1. Je wazo lako linawezekana kutokea (Is the idea feasible?)
2. Wazo lako linaweza kuleta mabadiliko/matokeo?
3. Wazo lako linaweza kudumu ? Linaweza kufanya kazi kwa muda mrefu na matokeo kuendelea kupatikana?
ANGALIZO: Kutokana na uzoefu nilionao, usiweke FEDHA/PESA kwenye equation ya mradi wako hasa kama unahitaji ufadhili. Miradi ya namna hii huwa inaleta mafanikio makubwa pale wadau wanapoona momentum ya mradi wako na namna mwekezaji atakavyoweza kuona faida ya muda mrefu.
Hivyo basi, ANZA na ulicho nacho.
Ushauri wangu:
1. Andika wazo lako liwe kwenye document moja nzuri sana inayoeleza kila kinachohusu mradi wako
2. Fungua blog au youtube channel halafu iendeshe vizuri (weka content nzuri na fikia watu wa kutosha)
3. Hudhuria events mbali mbali ambazo zinaweza kuhusika na unachofanya. Hii itakuongezea exposure, publicity na kukutana na watu ambao wataweza kuwa ngazi ya kuinua mradi wako.
Mimi naweza kukusaidia kwenye uandishi na kukupa mwongozo kwa hizi hatua za awali kama utapenda. Kwenye uandishi hapo WENGI huwa wanapata tabu kidogo kwa kuwa wengi huandika kama taarifa, yaani kama report ya field. Mradi kama huu unahitaji "strategic writing", yaani atakayekuwa anasoma kuna point za muhimu anapaswa kuziona bila kusoma sana na pia aone point hizi zinavyoungana kwa factor ya "effort, time na expected result".
Baada ya hapo, document hiyo ifanye kuwa mwongozo wako kwenye utekelezaji wa mradi wako day by day, ambapo itakusaidia kuendelea kufanya mradi kwa misingi uliyoweka pia kuboresha wazo kadri muda unavyokwenda. Then unapopoleka wazo lako kwa wafadhili kwa kuambatanisha na document yako, ni rahisi kuona na kuthibitisha kuwa kile ulichokipanga na unachokifanya (wazo na utekelezaji) vinaendana. Hapo kunakuwa na asilimia nyingi za kupata uufadhili.
Ila katika yote umekuja na wazo jema, naamini lengo ni zuri na naamini ukifuata njia sahihi utafanikiwa. You have my support 100% stay positive haya mambo yanawezekana.