MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Mimi nawashangaa sana wanachama CHADEMA na wafuasi wao kwa ujumla kulalamika mitandaoni kwa kukamatwa kwa sababu ya kudai katiba mpya, katiba mpya duniani kote hupatikana kwa maumivu makali sana yanayoambatana na watu kuumizwa na hata wengine kupotea.Kama mnadai katiba mpya haifikirii haya bora muache kucheza sarakasi zenu.
Itazameni katiba ya Kenya iliyopatikana baada ya maumivu makali ya 2007, itazameni katiba ya Afrika kusini iliyopatikana baada ya maumivu makali vile vile. Hizi katiba kwa sasa zinasifiwa kua ni bora kwa ukanda huu wa Afrika. Katiba ya Zanzibar ilipatikana vipi hadi kufikia kua na serikali ya umoja wa kitaifa?
Mnashindwa kuelewa kua na asilimia ya katiba ni makubaliano na maelewano baada ya watu kuumizwa ndipo wakae mezani wakubaliane. Hakuna katiba rahisi, JK alikwama kwa sababu njia iliyotumika ya kuipata katiba mpya ilikua si ya kawaida na pengine ingefanikiwa Tanzania tungevunja rekodi ya dunia.
Watawala hawako tayari kuunda katiba iwapunguzie power, eleweni hivyo.Hii bit ya kujenga uchumi kwanza ni geresha na Hadaa kwa wananchi wenye akili ndogo.