Kupauka kwa rangi ya gari ni kosa?

Kupauka kwa rangi ya gari ni kosa?

georgeallen

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
4,118
Reaction score
1,875
Leo nimekamatwa na traffic police nakuandikiwa risiti nilkalipe elfu 30 kisa rangi ya gari yangu kwenye bonnet imepauka.

Nilipomuuliza kupauka kwa rangi kunahatarisha vipi usalama wangu na wengineo barabarani akaniambia nikilipia ndiyo nitajua. Je, kupauka kwa rangi ya gari ni kosa? Na kama ni kosa ni sheria ipi inahalalisha kosa hilo?
 
Ulitakiwa ukatae kulipa ili akupeleke mahakamani.
Niliwahi kukamatwa kwa kosa "eti wheel cap imefungwa kwa wire"

Baada ya kubishana sana kwenye kulipa, nikaona bora tu twende kituo kikuu.Tulipo kuwa njiani nilimpigia mkuu wake, akanishauri anipeleke mahakamani hiyo kesi itamuangukia yeye mwenyewe mkamataji, bahati mbaya ni kwamba yule afande alisikia maongezi yetu.

Akaanza kulalamika kuwa nimemsemelea kwa boss wakati lilikuwa ni suala la kuelewana sisi wawili tu.

Tulipo fika kituo kikuu akaniruhusu niondoke kwani aliniomba msaada wa kumpeleka kituoni tu. "Kesi" ikawa imeishia hapo.
 
Jamaa wanatumia madaraka na dhamana yao vibaya sana aisee. Maana hapo ukihoji sana utaambiwa twende ukalale Central then ukasimame mahakamani!
Mie kuna siku maeneo ya External, taa ya kijani inawaa hata kublink haijaanza, nikapigwa mkono na askari. Akaambia nimeunganishia taa. Tulibishana sana mwishowe akanambia twende pale polisi post kwao then ifunguliwe kesi ambayo nitajibu mahakamani. Ilikuwa ni ijumaa hiyo. So hapo ilikuwa nilale ndani hadi j3.
Nilitoa 30K ila kila nikikumbuka roho yaniuma hadi leo. Ilikuwa mwaka juzi hiyo kesi.
Shida ni kwamba hata kama uwe innocent, yeye upande wake hawajibishwi kwa usumbufu alokuletea. Kuna haja ya kureview hizi sheria ili kuboresha weledi na utendaji wa hawa jamaa.
But pole sana mkuu
 
Ilibidi iwepo namba maalumu kwaajili ya wananchi ili tunapoonewa na traffick basi tupige ili tupewe msaada maana wakati mwingine sisi ambao hata huko polisi hatuna tunaemjua tunaishia kulipa faini hata tukiambiwa kosa letu ni kuendesha huku tumevaa miwani
 
Mimi huwa sipendi mazoea nao...hata wakiniomba lifti nawaambia gari imejaa...wakisema siti zipo tupu nawaambia kuna majini yangu nimeyabeba nyie hamyaoni
wanakera sana...wamezidi kuonea na ndiyo maana wakistaafu wengi wao wanaishi vibaya sana....hata watoto wao wakienda shule hawafanikiwi....hao watu wamejaa laana za malalamishi ya watanzania wenzao
 
Mimi kuna mama mmoja mweusi alishanilipisha faini pale sayansi sijawah kumsahau.... nilikariri adi namba yake ile ya WP... wanakosaga utu kabisa wakati mwingine utadhani wao sio watanzania wenzenu mnaoishi nao kwenye jamii
 
Nadhani ilikuwa mwaka juzi, mkuu wa Polisi alitoa angalizo kadha wa kadha. Moja wapo ya angalizo lilikuwa linaelezea askari hawezi kukukamata au kukupiga fine kwa sababu ya gari lako kupauka.

Nimejaribu kuangalia hiyo document lakini sijaiona, ila ipo.
 
Jesus Christ.....[emoji53] [emoji53] [emoji53]
Don't force the colour to fulfill your needs....[emoji45] [emoji45] [emoji45] [emoji45]
 
Mimi kuna mama mmoja mweusi alishanilipisha faini pale sayansi sijawah kumsahau.... nilikariri adi namba yake ile ya WP... wanakosaga utu kabisa wakati mwingine utadhani wao sio watanzania wenzenu mnaoishi nao kwenye jamii
Mkuu huyo mama ukikaa vibaya anatiaga na makofi ya uso nmeshuhudia mara kadhaa
 
Back
Top Bottom