georgeallen
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 4,118
- 1,875
Leo nimekamatwa na traffic police nakuandikiwa risiti nilkalipe elfu 30 kisa rangi ya gari yangu kwenye bonnet imepauka.
Nilipomuuliza kupauka kwa rangi kunahatarisha vipi usalama wangu na wengineo barabarani akaniambia nikilipia ndiyo nitajua. Je, kupauka kwa rangi ya gari ni kosa? Na kama ni kosa ni sheria ipi inahalalisha kosa hilo?
Mimi huwa sipendi mazoea nao...hata wakiniomba lifti nawaambia gari imejaa...wakisema siti zipo tupu nawaambia kuna majini yangu nimeyabeba nyie hamyaoniIlibidi iwepo namba maalumu kwaajili ya wananchi ili tunapoonewa na traffick basi tupige ili tupewe msaada maana wakati mwingine sisi ambao hata huko polisi hatuna tunaemjua tunaishia kulipa faini hata tukiambiwa kosa letu ni kuendesha huku tumevaa miwani
Mimi huwa sipendi mazoea nao...hata wakiniomba lifti nawaambia gari imejaa...wakisema siti zipo tupu nawaambia kuna majini yangu nimeyabeba nyie hamyaoni
wanakera sana...wamezidi kuonea na ndiyo maana wakistaafu wengi wao wanaishi vibaya sana....hata watoto wao wakienda shule hawafanikiwi....hao watu wamejaa laana za malalamishi ya watanzania wenzao
Mkuu huyo mama ukikaa vibaya anatiaga na makofi ya uso nmeshuhudia mara kadhaaMimi kuna mama mmoja mweusi alishanilipisha faini pale sayansi sijawah kumsahau.... nilikariri adi namba yake ile ya WP... wanakosaga utu kabisa wakati mwingine utadhani wao sio watanzania wenzenu mnaoishi nao kwenye jamii
Ni kosa kubwa mno maana viwanda vya rangi nchini vinakosa biashara