04.11.2020, Saa nne usiku:
Kwani uchaguzi si umeisha?
Kwani ushindi wa ‘kishindo’ si tayari?
Kwani ‘watu wengi’ si wanawakubali?
Kwani maandamano si yameshadhibitiwa kwa nguvu kubwa?
Sasa nini sababu ya kuendelea kuminya minya mitandao ya kijamii na ‘kutupimia kwenye vijiko’?
Hivi wanajua athari za kuminya mitandao kwa wiki nzima?
Hivi hawajui kwamba mitandao sasa ni biashara, ni uchumi, ni maisha?
Nani atafidia wale wote ambao biashara zao zimeathiriwa pakubwa?
Nani awaponye wale wote ambao wameathiriwa kisaikolojia kwa kubaniwa mitandao?
Kupenda mambo ya gizani ni uovu, ni dalili ya uchawi!