Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
1. Je, ninajenga nyumba yangu au naibomoa?
2. Je, ninawekeza kwenye ndoa yangu? Natumia uwezo wangu kuiboresha?
3. Je, naonyesha kumthamini na kumjali mume wangu?
4. Je, natumia nguvu zangu na uwezo wangu kwa ajili ya familia yangu?
5. Je, natengeneza mazingira kwa maneno na matendo yangu yakumfanya mume wangu afurahie na kupenda kuwa nyumbani?
6. Je, naridhika na kuihudumia familia yangu?
7. Je, hisia zangu na upendo wangu ni kwa ajili ya mume wangu au mtu mwingine? Je, muonekano wangu, maneno mazuri na ushawishi mwema ni kwa ajili ya mume wangu au watu wengine?
8. Je, natimiza mahitaji ya mume wangu?
9. Je, ni mwaminifu kwa mume wangu? Nina uhusiano wowote wa siri ambao sitaki mume wangu ajue?
10. Je, mume wangu yupo huru kuwa muwazi kabisa kwangu hata kunikosoa?
11. Je, ninaruhusu mawazo ambayo siyo safi kuwa ndani yangu kupitia redio, televisheni au vitabu?
12. Je, nimekuwa kimbilio na faraja kwa mwanaume ambaye ndoa yake ina matatizo?
13. Je, natafuta ushauri na faraja kutoka kwa mwanaume mwingine (mchungaji, kiongozi wa kanisa, mshauri, mfanyakazi mwenzangu) na sio mume wangu kwanza?
14. Je, ninauhusiano wa karibu zaidi na mwanaume mwingine kuliko nilivyo na mume wangu?
15. Je, nimekuwa mkali na mwenye maneno yasiyo ya upole au ni mwenye maneno mazuri na yenye upole na unyenyekevu?
16. Je, naonekanaa rahisi rahisi kwa wanaume wengine au naonekana ni mtu mwenye msimamo? Je, naruhusu mizaha isiyofaa na watu wengine?
17. Je, kuna kitu katika mavazi yangu, muonekano au maongezi ambacho kinaweza kuwa kichocheo kwa wanaume kuwa na tamaa?
18. Je, ninavyoongea na wanaume kazini au popote naonyesha kuwa mimi ni mwanamke wa kristo au nakuwa nawaonyesha upendo na ukaribu wa kupitilizia ambao unapaswa uonyeshwe na wake zao?
19. Je, nimeweka mipaka katika mahusiano yangu na watu wa jinsia ya kiume? Ni mipaka gani hiyo?
20. Je, kuna mausiano niliyonayo ambayo yanaweza kuleta utata kwa watu?
21. Je, mume wangu na watu wengine wanao nifahamu wanaweza kusema kuwa mimi ni mwanamke mwenye busara na anayejiheshimu?
22. Je, nimeazimia moyoni mwangu kuwa safi mbele za Mungu? Je, ni mfano wa kuigwa na wanawake wengine wanaoishi maisha ya kumfuata Mungu?
Mithali 31:10 Mke mwema, ni nani awezaye kumuona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
PRINT HII KARATASI MPELEKEE AJIBU MASWALI YOTE HAYO HAPO JUU TENA WEWE UKIMUULIZA MWENYEWE