Kupiga bibi jamani si ustaaarabu!!!!!!

chiko

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2010
Posts
590
Reaction score
271
Nimeshuka wanajamvi baada ya kukaa manyasini nikichungulia chungulia jamvi. Nimejaribu kujiuliza bila ya kupata jibu, hivi katika karne hii bado kuna mababa wanapiga wake zao!!.

Imenitokea mimi mwenyewe binafsi, ikabidi nihame nyumba, sababu jirani alikuwa na tabia mbaya ya kutwanga mke, natumai mwanipata..sio eti kuchapa vibao ama kuchapa mijeledi, laa kupiga na nia ya kuuuaa magumi mateke, jamaa anakanyaga kama ataka washa bajaj.
Ilikuwa usiku mmoja jamaa jirani(Mtu na heshma zake,ofisaa fulani wa Benki,sio eti vijana hawa wakihuni) kaingia nyumbani baada ya kutoka ulevini, majira ya saa za manane, twasikia mayowe na vurumai!!, Kama majirani wema tumetoka kusaidia. Mara twagundua bwana apiga bibi. Hasira zikanipanda nikataka kuingilia lakini mwenzangu akaniambia "watu walalao Blanket mmoja mambo yao usiiingiliee", nikapoesha hasira, na kwa kweli baada ya masiku kidogo hivi niliona majirani hao hao wameshikana mikono watoka shopping.......Daahhhh nilihama mtaa huo.

Nimekuwa mpaka mtu mzima, sikuwahi kuona Baba yangu na Mama wakipigina, sasa imagine hio "Trauma", kawaida mimi ni mtu mtulivu lakini nachukia sana maonevu!!!!

Jamani...Hata kama ni itikadi zetu, (kuna makabila, bila kutaja yana mambo haya), jamani wana JF, kama kuna waume wenye tabia kama hizi humu, jamani wacheni tuwe wastaraabu. Kuna njia mbadala za kusuluhisha migogoro ya nyumbani sio KUPIGAAAAA......GrrrrRRRRRRR
 
ndo maana mimi nimeamua KUCHUKUA KOZI KWA FRANCIS CHEKA...mapemaaaaaaaaa:car:nawai koz cu u francis ananisubiria darasan...
 
 
natamani kupata mpenzi anayepiga hahahahahaaa!!!
 
sisi wakurwa huwa atubigi, ni muendelezo wa mila, utamaduni & desturi.
 
 
ha ha ha!
Ukipewa kipondo siku hiyo adhabu yake hapati unyumba. Lol!
Mapumziko ya nguvu.

unafikiri kwa nini namtamani anayepiga,maana kitakachompata hatakaa akisahau maishani mwake ukizingatia nna mikono minneπŸ™‚
 
kupigana kunatokana na shetani tu. kila mtu anaweza kumpiga mke wake kama moyoni mwake hana Mungu bali anaye shetani mchafu...roho chafu inaweza kuiendesha familia na kuipinduapindua ipendavyo...na kuna watu wengine wanapigana kwasababu wamepagawa na roho chafu hat akama wao hawajijui....habari ndo hiyo...karibu kwa Yesu, muokoke mponye ndoa zenu.
 
ha ha ha!
Ukipewa kipondo siku hiyo adhabu yake hapati unyumba. Lol!
Mapumziko ya nguvu.

kumbe hujui, wengine unyumba mtamu wakiwa na manundu,,,,,,πŸ™‚πŸ™‚
 
kumbe hujui, wengine unyumba mtamu wakiwa na manundu,,,,,,πŸ™‚πŸ™‚

Mhhh hapo yaweza kuwa kweli, nasikia wengine baada ya magumi na mateke, ndio kwaandaliwa mechi ya KUFA MTU hadi cheeee!!!
 

kula tano mkuu..hiipost imenifurahisha sana kwa sababu mimi mwenyewe nipo agaisnt sana na hii kitu
 
Jamani sie wengine bila kupigwa unaona hupendwi
 
mmhh hii mbaya sana..
nimeona na nimeshuhudia ..

kweli kweli jamani sijui watu wengine wanawazaga nini tu.
halafu baadaye anasigizia ni shetani alinipitia..
au samahani nilikuwa nimelewe..

yaani CHIKO natamani nikupe senks zaidi ya 100 kwa ajili ya hii thread..
hopeful wengi wataisoma..
asante sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…