Jamani naomba msaada. Maana huwa napiga chafya sana kila ninapohisi kunusa vumbi, mtu akivuta sigara moshi tu ukipita mbele yangu, pia kama natafuta nguo kabatini, nikipulizia pafyumu n.k. Chafya hiyo huambatana na mafua mepesi. Naomba mwenye kujua dawa yake nifanyaje maana hospitali huwa napewa piliton, chengachenga n.k bila mafanikio.
yani we acha mimi ni hivyo hivyo nimemaliza hospitali zote lakini wapi kuna hospitali hapo magomeni nilienda wanashughulika na mambo ya allergy and wanaku hakikishia unapona kbs lkn wapi wanataka ukienda pale ni kazi kununua midawa kwa midawa na masharti ya vyakula, mi ilinianza i think nilivo kuwa 13 kitu kama icho,bibi yangu kaniambia hili tatizo linaitwa KAMBAKU,kuna dawa yake au nenda kwa wamasai ulizia mavumba ya kambaku unakoroga na chai kidogo afu unakuywa kama pua zimebana unanusa unapiga chafya zizibuke, lakini nisikukatishe tamaa once ukiacha or ukisahau kunywa mafua yako palepale, the only way i cope with it nimejifunza kuishi nayo nimeacha kupulizia perfum na body spary,sabuni natumia ya punda ile ya blue na white, nikiwa nafanya usafi au natafuta nguo kabatini i hold my breath au najifunga kitambaa afu sasa mimi nakaa karibu na barabra so vumbi ndani ni lazima kabla ya kulala kun'guta kitanda mafua yakicharuka kula machugwa as much as you can mi ata 7 nakula na kabla ya kulala meza panadol, dah yani tabu tunayo pata watu hawajui tu wanaona kaa mafua ya kawaida wakati same times maskio yanaziba, ukiinama kichwa kinauma, maeneo ya nyusi kunauma, milago ya pua inauma mwili wote unaskia homa, yani siku nzima unakuwa huna raha, ila bibi yangu kaniambia ukitaka yapone ni kwenda kwa mganga sijui akupikie chungu afu unajifukiza naskia unapewa mashrti ya vitu ambovo usile for like a week then unapona kabisaa,sasa sijui kama ni kweliJamani naomba msaada. Maana huwa napiga chafya sana kila ninapohisi kunusa vumbi, mtu akivuta sigara moshi tu ukipita mbele yangu, pia kama natafuta nguo kabatini, nikipulizia pafyumu n.k. Chafya hiyo huambatana na mafua mepesi. Naomba mwenye kujua dawa yake nifanyaje maana hospitali huwa napewa piliton, chengachenga n.k bila mafanikio.