Kupiga honi mahakamani na hospitali ni kosa?

Kupiga honi mahakamani na hospitali ni kosa?

andrewk

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2010
Posts
3,102
Reaction score
489
Najarijubu kujiuliza sehemu nyingi za mahakana au hospitali mi marufuku kupiga honi ya gari, na ukukaidi amri hii unaweza kushitakiwa na kuhukuniwa kufungwa au kulipa faini........

sasa kwa uelewa wangu kidogo, kwa hospitali ni kuepusha usumbufu kwa wagonjwa. Mahakamani je? hivi watu wenye taaluma hii tu ndio hawatakiwi kushumbuliwa, au kuna nini cha ziada? ..... naomba msaada wenu
 
Ni hoja nzuri umejenga kwamba huenda hata hospitali kuwe na sheria ya kutopiga honi.......lakini kwa ujumla wake makelele yasiyo na tija yanaangukia wenye sheria za madhara/kero (torts) au jinai kulingana na uwasilishaji na kwa taarifa yako siyo hospitali hata majumbani, iliwahi kuletwa hoja hapa juu ya baa kujengwa kwenye makazi ya watu, kosa la kisheria hapo ni pamoja na noise polution.....kwa hiyo hata nyumbani unaweza kujenga hoja......jaribu kutafakari ukumbi wa Amana na Hospitali ya Amana pale, ikiwa mtu atajitokeza na kujenga hoja, hospitali itakuwa na uzito zaidi......japo pia pataangaliwa aliyekuja baadaye ni yup ukumbi au hospitali any way ni kazi ya mahakama itakuwa hiyo........kwa wenzetu mf. Uingereza hata kulia tu penye msiba ni kero kwa jirani sembuse kupiga honi kwenye nyumba yako mwenyewe..mlio huko mtujuze zaidi.....

Kwa shauri ulilotea kama alivyodokeza mchangiaji Dadio hapo juu hii inaitwa kuidharau au kuingilia uhuru wa mahakama (court contempt) rationale ni kwamba mahakamani panatakiwa pawe na uhuru wa kutosha ili kutoa umakini wa kusikiliza pande husika, kwa hiyo kitendo cha kupiga honi au kufanya matendo yoyote yale ambayo yatavuruga umakini huo (kucheka, kusikiliza simu, kunong'ona na mwenzio etc)hukumu yake ni ya pao kwa pao (sumary trial) kwani endapo hili lingeachiwa basi huenda kitendo cha kugeuza akili ya umakinifu kikawa na madhara makubwa sana kwa maamuzi ya mahakama kutotenda haki.....(kumbuka katika kanuni za haki ni heri uachie huru watu kumi wenye makosa kuliko kumtia hatiani mtu mmoja ambaye hana hatia) ni kanuni muhimu sana hivyo ni pamoja na mazingira kama hayo......japo uelewe pia kwamba to every rule there is an exception mfano mtu akikohoa mahakamani kwa kupaliwa itakuwa ni utetezi kwamba alikua havurugi ule usikivu wa mahakama..etc, hivyo ikiwa utetezi ni kwamba ililzimika kupiga honi kuokoa maisha ya mtu mathalani aliyekuwa anavuka barabara eneo la mahakama (na ikathibitishwa hivyo).......lakini kila shauri litaamuliwa kulingana na mazingira na utetezi

Nimejaribu japo mm si mwanasheria
 
nyongeza: siyo hospitalini na mahakamani tu. sheria za traffic zinakataza Hata ukiwa barabarani (ambapo hospitali na mahakama hazipo karibu) kupiga honi unnecessarily/bila sababu ya msingi. Faini ni Tshs 30,000/ au kifungo.
 
Back
Top Bottom