Raha ya mke kupigwa na MUMEWE kawaulize Wakurya. Unataka wiki nzima ipite bila mzee kumpiga mkewe, hujui kupiga mke ni chachandu ya kudumisha ndoa? Sikiliza, mama mmoja alipofiwa na mume ambaye kila mara alikuwa anagawa kipigo, mama yule alirithiwa na shemeji yake ambaye alikuwa mpole sana na hakujua kupiga. Yule mjane alionekana kila mara kwenye kaburi la marehemu mumewe akililalia na kujigaragaza pale kaburiki huku akilalamika kwamba anakumbuka vipigo vyake kwani sasa aliyemrithi ni kama wameoana wanawake watupu. Alipotonywa mrithi yule mambo ya mke mpya, alienda makaburini mwenyewe na kweli akajisikilizia mwenyewe maneno ya bibi yule akilia kwa sauti kuu kukumbuka vipigo. Yule bwana jioni ile aliteremsha kipigo kwa mama huyo, mama akapiga kilio kikubwa kijijini pale watu wote wasikie kwamba sasa amegundua kwamba mrithi wake kumbe naye anampenda! Upo hapo? Kuna kupiga unakoweza kuombwa tena "Niongezee tafadhali" lakini kuna kipigo cha mbwa mwizi ndio hakifai. Daima kofi la mpenzi haliumi, vijana jifunzeni hilo.
Kipigo kipo cha aina nyingi, unaweza kumpiga mkeo kwa kipande cha Wax au khanga yenye maneno mazuri, au kwa paja la kuku na kumtoa mwende mbali kidogo mkakae chini ya "kivuli" kumalizia mambo yenu, mkaimba nyimbo zote hadi mkome ubishi. Naye mkeo anayo haki ya kukudunda kwa shati la "EAGLES" au "Kampunyoko" yaani vile vitambaa wanavyotia rangi mitaani nimesahau jina la mjini. Na kadhalika. Kipigo cha mbwa mwizi sio cha mapenzi bali hasira na hapo tena sio chachandu ila sumu. Muliyo wamayu na watate?