Mimi sio magari tu, hata nyumba kali huwa sipendi shobo nazo kupiga picha.
Hata Mlimani City siingii, achana na kupiga picha kule. Siwezi toka hapa niende kupeleka mikojo yangu kwenye ofisi za watu na hakuna kitu naenda nunua. Nikienda sehemu nakuwa nahitajika, nikipiga picha na kitu huwa kinanihusu.
Mimi najua class yangu na ndo nakaa nayo, nahangaika kutoka na najua ni suala la muda tu. Unakuta mtu anajikomba kwa marafiki zake walioenda Singapore, India, SA, Canada. Akipata shida au akiwa na event hawana shobo nae.
Unakuta mtu anajizungusha na mademu wakali ila mara zote anadate na kina miss Buza tu.
Ni sawa na hizo gari, pata shida ya kwenda hospitali uone kama kuna Mark X au Subaru itatoka uko kukubeba. Utabebwa na bajaj ukibahatika ist.
Huwa sina kiherehere na vitu vya level ya juu yangu.
NB: Nawasema wenzangu na mimi ambao wengi humu hawapo. Humu wengi wana magari na maisha mazuri.