Kupiga plasta au ripu ni kazi inayotakiwa kufanyika kwa umakini mkubwa ili kazi ya umaliziaji yaani finishing iwe katika viwango bora

Kupiga plasta au ripu ni kazi inayotakiwa kufanyika kwa umakini mkubwa ili kazi ya umaliziaji yaani finishing iwe katika viwango bora

Kicheche mkali

Senior Member
Joined
Nov 3, 2021
Posts
160
Reaction score
141
#kelv

Habari!

Umeshajenga na umefikia hatua Ya kupiga Plasta au Ripu, fuatana na mimi nikupe faida!

KUPIGA PLASTA AU RIPU NI KAZI INAYOTAKIWA KUFANYIKA KWA UMAKINI MKUBWA ILI KAZI YA UMALIZIAJI yaani Finishing iwe KATIKA VIWANGO BORA

Ili kazi ya kupiga ripu/plasta ifanyike kwa urahisi, kwa ufanisi na hata kwa gharama ya wastani wa kawaida inabidi kazi zinatangulia za kujenga nguzo na kuta ziwe zimefanyika kwa usahihi mkubwa....,

Ikiwa kazi hizi hazikufanywa kwa ufanisi unaotakiwa kazi nzima ya kupiga Plasta huwa ngumu na kubwa na itahusisha gharama kubwa sana ili kuweza kulirudisha jengo katika hali nzuri.

Kabla ya Kupiga plasta Jengo lako hakikisha saiti ni safi kwa maana ya mazingira yake ili kuokoa udongo na saruji ambayo itatumika kupiga plasta visipotee kwa kiwango kikubwa....

Anza kwa kuweka timanzi kwenye ukuta wote na nguzo zote Yaani timanzi iwekwe kwenye ukuta kwa kutumia vifaa maalum vya kutafutia usawa kwenye ujenzi....Tumia KOBILO KUWEKA hii Mota au Timanzi ili plasta yako iwe inafuata vipimo hivyo kwa kunyooka.....

Baada ya kuweka Timanzi sasa unaweza kuanza kupiga Plasta yako kufuatana na vipimo ulivyojiwekea....

Umakini mkubwa huanzia kwenye setting ya jengo ndani ya msingi(setting out) kisha kutumia vipimo na vifaa vizuri vya kunyoosha na kuzingatia pembe au kona zote na vipimo sahihi pamoja na ufundi bora ambao utapangilia kila kitu katika usahihi mkubwa pamoja na vifaa vya ujenzi kama vile tofali zenye viwango bora sana na zenye ukubwa unaolingana.

Kwa kuzingatia haya kazi ya Skimming na Rangi inakuja kuwa nzuri, rahisi na yenye ufanisi mkubwa......

Kwa mahitaji Yote Ya Ujenzi kuanzia chini hadi kukukabidhi Funguo wasiliana nasi kwa namba hii 0789005562....

Ushauri na bei za vifaa pamoja na Ufundi Tafadhali Tupate kwa namba hizo juu! Au kwa link hii

Wa.me/255789005562

Njoo Tujenge pamoja na tumalize pamoja!

Popote Tanzania tunakufikia....

By

Kelvin Hk
FB_IMG_1736754039777.jpg
FB_IMG_1736754044847.jpg
 
Hongera sana ...vp nikitaka screen nzuri nahitaji kupiga plasta gani
 
Back
Top Bottom