upimaji mbegu za kiume unaitwa male factor au Seminalysis. Huwa zinatakiwa shahawa za mwanamme kwenda kupimwa. Masharti: kabla ya kuchukua shahawa,mwanamme anatakiwa asiwe ame sex na kumwaga shahawa kwa siku 4-5. Lengo ni kupata shahawa zenye mbegu zilizokomaa. Inatakiwa lisivuke muda wa saa 1 toka umezipata shahawa na kuzifikisha maabara hivyo JIPANGE jinsi ya kuendana na muda huo.Wakati wa kuzipeleka,zinatakiwa zisipate ubaridi wowote bali zipate joto la mwili,hivyo unashauriwa uhifadhi kichupa cha mbegu aidha kwapani au kati ya mapaja(hapa napo JIPANGE).Njia kuu za kupata shahawa ni mbili.1. Kufanya mastabesheni na kumwagia goli la kwanza kwenye kichupa maalum utakachopewa. 2. Kufanya mapenzi namkeo,na kuwa makini kuchomoa dushe na kumwaga shahawa za goli la kwanza kwenye kichupa maalum utakachopewa. Kumbuka ni shahawa za bao moja la kwanza tu ndio zinatakiwa. Majibu kwamba mbegu zipi ni bora ni ya kitaalamu zaidi na nikiweka hapa tutajaza seva lakini huwa zinaangaliwa uwezo wa kuogelea ukeni,ubora wake,PH yake nk. Mengineyo dokta wako aweza kukufafanulia. Kama kuna mengine sensitive wataka jua,ni PM.