Kupimiwa kiwanja cha kujenga kituo cha mafuta

Kupimiwa kiwanja cha kujenga kituo cha mafuta

Habari wakuu, naomba process ya kufanya mpaka unapimiwa eneo lako la biashara kufungua kituo cha mafuta, na aina ya makampuni yanayopima maeneo tafadhali.
Je eneo husika lipo kwenye Ramani za mipango miji?
 
Habari wakuu,

naomba process ya kufanya mpaka unapimiwa eneo lako la biashara kufungua kituo cha mafuta, na aina ya makampuni yanayopima maeneo tafadhali.
Inatakiwa kuchukua coordinates a kuzipeleka Ardhi kujua kama eneo limepangwa kwa matumizi gani, kama litaruhusu shughuli husika. Mbali na survey Pia utahitaji kufanya Environmental Impact Assessment (EIA) kwaajili ya NEMC.
Tuwasiliane mkuu Nicheki kwa whatsapp namba 0717682856 tufanye kazi kama members jf
 
Nenda kwa Mpima ardhi ktk Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya eneo lililopo na kuambatanisha vielelezo vya umiliki.

Atakuelekeza uandike barua kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya husika
.
Utapewa Mpima na atakwambia uende ofisi ya serikali za mitaa kujaza form na wapakani.

Taratibu nyingine zitafuata za kupima kisha kupelekwa wizarani.

Lakini labda iwe bahati yako vinginevyo urasimu ni mkubwa sana kuliko maelezo.

Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom