macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 29,500
- 61,451
soma hapa kwa kirefuNdugu zangu wana JF, naomba kuelemishwa ni nin hatima ya mbunge anayepita bila kupingwa hapa nchini. Nafahamu kuwa, kila chama kina mchakato wake wa kuteua mgombea wa ubunge wa jimbo, hii ikiwa ni pamoja na kuitisha kura za maoni, na baadaye kuchakachua matokeo na kumpitisha aliyeshinda au yule ambaye chama kiinampenda (si lazima awe mshindi). Sasa, pale inapotokea huyo mshindi wa chama kimoja anakuwa ndiye mgombea pekee, baada ya vyama vingine kupata mgombea au wagombea waliojitokeza na kupita kuamua kujitoa kwa njia yoyote ile, au wagombea kuwekewa pingamizi na kutolewa; ni nini hatima ya huyu mtarajiwa aliyepita bila kupingwa na hivyo hakuna uhakika kama anapendwa jimboni mwake:
(1) JAnaweza kuteuliwa kuwa waziri?
(2) Anaweza kuteuliwa kuwa waziri mkuu?
(3) Je anaweza kugombea Uspika?
Naomba nisilaumiwe, bali nielimishwe!! Huwezi jua, inawezekana tuko wengi tu tusioelewa suala hilli!! Nawasilisha.
Mbunge anayepita bila kupingwa - mmmmmmmmmmmmmm
Nadhani si halali hatimaye kumwita huyu mbunge wa kuchaguliwa. Yeye kapitishwa na chama chake tu. Hakuchaguliwa na watu. Ni vigumu hata kuelewa kwamba atawakilisha watu wa jimbo husika kwani hawakumpigia kura. Ni mbunge atakayewakilisha chama chake kilichomteua - sio wanajimbo. Naamini kuna kasoro kuwa na wabunge wa namna hii.
PART III FINAL NOMINATION OF CANDIDATES FOR PARLIAMENTARY ELECTIONS
44. Unopposed Candidates Act No. 6 of 1992 s 19 Act No. 8 of 1995 s 6.
Where only one candidate is nominated for an election in a constituency such candidate shall be deemed to be elected and the commission shall, by notice in the Gazette declare him to have been elected.
Mwanakijiji,
Until I actually read the law I thought this was either a mere precautionary measure or a case of misinterpretation on your part.
Then I went and read the 2005 law from the above given link, and it hit me with a BANG!
I am still hoping against hope that someone can correct us all with a more sensible update to this imbecilic law. Why isn't the press drumming this injustice up ?
Mzee Mwanakijiji, asante kwa hili. Hii ni hoja ya nguvu iliyobeba nguvu ya hoja ambayo kisheria, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, haina mahali pa kuipangulia.
Ila kila sheria huwa inatungiwa regulations za utekelezaji wa sheria husika, sijabahatika kuziona regulations za mwaka huu, ila kwa mwaka 2005, kwenye regulations, zilimpa mamlaka msimamizi wa uchaguzi (RO) kumtangaza mgombea aliyepita bila kupingwa kuwa tayari ni mbunge/diwani mtarajiwa. Kitu ambacho bado sijakijua, hiyo regulation ili derive wapi mamlaka hayo ya kiimla!.
Regulation hiyo ilisema iwapo hakuna upinzani kwenye nafasi ya urais, mgombea aliyejitokeza, atapigiwa kura za ndiyo au hapana, kama enzi ya chama kimoja, kuweka sura na kivuli., sijui kwa nini utaratibu huu, usitumike, kwa hao wanaodaiwa kupita bila kupingwa.
Kwa kawaida kabla ya uchaguzi, document ya regulations ndio hutoka kwanza, na vyama vyote lazima visaini hizo rules of the game,ndipo kipenga kipulizwe, kwa vile kipenga kimeshapulizwa, na wakuu wa vyama vyote wameshasaini kanuni za mchezo, nadhani, there is nothing that can be done to rectify this serious anomality ili ni hoja muhimu ya kuishikia bango, katika madai ya tume huru ya uchaguzi.
Asante tena.
Pasco.
Katiba ya Tanzania ya 1977 ipo wazi kwamba mbunge ni wa kuchaguliwa na hakuna mbunge wa kupita bila kupingwa.Ndugu zangu wana JF, naomba kuelemishwa ni nin hatima ya mbunge anayepita bila kupingwa hapa nchini. Nafahamu kuwa, kila chama kina mchakato wake wa kuteua mgombea wa ubunge wa jimbo, hii ikiwa ni pamoja na kuitisha kura za maoni, na baadaye kuchakachua matokeo na kumpitisha aliyeshinda au yule ambaye chama kiinampenda (si lazima awe mshindi). Sasa, pale inapotokea huyo mshindi wa chama kimoja anakuwa ndiye mgombea pekee, baada ya vyama vingine kupata mgombea au wagombea waliojitokeza na kupita kuamua kujitoa kwa njia yoyote ile, au wagombea kuwekewa pingamizi na kutolewa; ni nini hatima ya huyu mtarajiwa aliyepita bila kupingwa na hivyo hakuna uhakika kama anapendwa jimboni mwake:
(1) JAnaweza kuteuliwa kuwa waziri?
(2) Anaweza kuteuliwa kuwa waziri mkuu?
(3) Je anaweza kugombea Uspika?
Naomba nisilaumiwe, bali nielimishwe!! Huwezi jua, inawezekana tuko wengi tu tusioelewa suala hilli!! Nawasilisha.