Pre GE2025 Kupita bila kupingwa kunapenyezwa taratibu na CCM, tutashtuka ya 2020 yakijirudia tena

Pre GE2025 Kupita bila kupingwa kunapenyezwa taratibu na CCM, tutashtuka ya 2020 yakijirudia tena

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kama mmeona sasa hivi upande wa CCM kila wakifanya mkutano kiongozi husika anapotishwa bila kupingwa kienyeji ama anaombewa kisayansi kupitishwa bila kupigwa!

Ilianza kwa Samia na Mwinyi, Diwani akataka Silaa apitishwa bila kupingwa, Rufiji nao wakampitisha Mchengerwa bila kupingwa na kwa Biteko leo limepenyezwa pia kisayansi!

Haya hayafanywi kwa bahati mbaya, kila kitu kimepangwa vizuri. Taratibu itaonekana kama kawaida kwa kuwa CCM wanafanya na watataka hili lifanyike hivyo hivyo kwenye Uchaguzi Mkuu, ya 2020 yajirudie tena. Baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa ovyo kuwahi kutokea Uchaguzi Mkuu utaenda kuwa wa kipuuzi zaidi.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Sheria ya uchaguzi imesema hilo limekoma 2020, hakutakuwa na kupitwa bila kupingwa tena kwanini lianze kupenyezwa sasa hivi?

Wnanatengeneza njia kwa wale vigogo serikalini kurudi wote serikalini 2025, wameona bila janja janja hawawezi kupita, tukemee haya mapema. Sheria isimamiwe.

Sina hakika hili likoje kutokana na katiba ya CCM Pascal Mayalla, Kiranga na wengine naomba mwongozo hapa.

Februari
 
Write your reply...
Tutafanya sasa na ndiyo wameamua liwalo na liwe hata kwa kumwaga damu,wako tayari
 
Write your reply...
Tutafanya sasa na ndiyo wameamua liwalo na liwe hata kwa kumwaga damu,wako tayari
Tukemee na kupinga haya sasa, tukikaa kimya inaonesha tunasapoti haya kuendelea
 
Walete tu Mgombea Binafsi angalau kuwe na another alternative apart from haya magenge...

 
Back
Top Bottom