SoC04 Kupitia mfumo huu bora wa elimu adui ujinga, maradhi na umasikini hawatatusogelea ng'o

SoC04 Kupitia mfumo huu bora wa elimu adui ujinga, maradhi na umasikini hawatatusogelea ng'o

Tanzania Tuitakayo competition threads

MombaDier

Senior Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
123
Reaction score
232
Ujinga, maradhi na umasikini ni maadui ambao wamekuwa wakiitesa nchi ya Tanzania na kati yao ujinga ndiye adui kuu anayewapa nguvu wengine. Maana mojawapo ya ujinga ni ile inayosema kuwa ni kitendo cha kukosa maarifa juu ya jambo fulani. Umasikini tulionao unasukumwa zaidi na ujinga tulionao haswa katika matumizi ya rasilimali tulizobarikiwa. Kitendo cha kukosa maarifa juu ya matumizi ya rasilimali zinazotuzunguka ni ujinga, kugundua sehemu zenye makaa ya mawe au madini ila tusijue namna ya kuyavuna nao ni ujinga.

Kukosekana kwa elimu kumetupelekea kuwa wahanga wa maradhi mengi kutokana na kukosa taarifa sahihi. Kumekuwa kukizushwa maneno mengi mtaani mfano hivi karibuni ilitolewa chanjo ya UVIKO-19 lakini maneno mengi yaliyopelekea kusuasua kwa zoezi yalizushwa na hatima yake walijitokeza watu wachache tofauti na matarajio.

Magonjwa kama vile kipindupindu hulipuka mara kwa mara kutokana na kukosa elimu juu ya namna sahihi ya kutunza mazingira yetu hali inayopelekea kusambaa kwa taka hatarishi ambazo zimekuwa zikitunza wadudu wasambazao magonjwa hayo.

Elimu ndiyo suluhu sahihi dhidi ya maadui hao sugu ila kwa mfumo wa elimu uliopo sasa siyo rafiki kwani unamtaka mwanafunzi awepo darasani kwa kipindi kirefu na kumnyima muda wa kujishughulisha na shughuli za kijamii zinazoweza kumjenga zikamuingizia kipato siku za usoni na kukabiliana naye adui umasikini pamoja na tatizo la ukosefu wa ajira unaomtaka mhitimu wa chuo awe mwenye uzoefu wa miaka kumi.

8:4:2/3:3 ndiyo mfumo ninaouzungumzia hapa yaani miaka minane (8) shule ya msingi, minne (4) shule ya upili(sekondari), miwili (2) shule ya juu ama mitatu (3) kwa wale wanaoamua kwenda vyuo vya kati na mitatu (3) ya mwisho kwa vyuo vikuu. Jambo la kushukuru ni kuwa wizara ya elimu imejitahidi kulitizama hili kwa kuja na mfumo 7:4:2/3:3 ingawaje bado hatujatibu tatizo tumelipunguzia makali tu.

Nasema hivyo kwa maana inaonekana ni shule ya msingi pekee ndiko muda unakopotea ila hata hizi ngazi za juu za elimu kuna muda mwingi unapotea. Kwa mfano katika ile miaka minne ya shule ya upili kuna mada inaitwa “Life skills” utaisoma kila darasa katika miaka minne utakayohudhuria, utakutana nayo kidato cha tano na chuo kikuu kwenye somo liitwalo development studies. Pia zipo hesabu zinaitwa “K.K.S na K.D.S” ukifika sekondari zitaitwa “G.C.F and L.C.M”. Lakini pia tuition za pre-class nazo hutupunguzia muda mno, vuta picha unamaliza darasa la saba unapelekwa pre-form one, unamaliza form four unapelekwa pre-form five alafu ukifika shuleni unafundishwa upya yaani kwa kifupi TUNAJIKABA.

Bado kuna uhitaji wa uingizwaji wa masomo ya ujasiriamali na ufundi ama vijana kumaliza mapema (wakiwa na umri mdogo) hali itakayopelekea kujifunza shughuli za ujasiriamali mapema kwa maana kuna umri ukifikiwa ni vigumu mno kujifunza hasa huu tunaomaliza nao siku hizi. Suluhisho juu ya hili ni kutazama ni kwa namna ipi muda wa kuwepo darasani ukapunguzwa ili iwe rahisi kukabiliana na adui umasikini baada ya kukabiliana naye adui ujinga kwa miaka kadhaa shuleni.

Inahitajika kuokoa muda unaotokana na kurudia kusoma mada ya aina moja ikiwezekana mfumo uliopo vyuoni wa kutoisoma tena mada uliyoifanyia mtihani baada ya kujifunza ndani ya kipindi cha miezi minne (yaani Semista moja) ukatumika kwa ngazi zote za elimu.
Sijamaanisha kuwa wanafunzi wa shule ya msingi wafundishwe hesabu za MAGAZIJUTO kwa miezi minne halafu wazifanyie mtihani ila kupitia mitihani ya darasa la nne, la saba, kidato cha pili, cha nne na kile cha sita inaweza kubaki vile vile.
Kitu cha kubadilisha ni kuwa mada iliyofanyiwa mtihani darasa la nne haina sababu ya kurudiwa kwenye mtihani wa darasa la saba na mada iliyofanyiwa mtihani wa kidato cha pili haina ulazima wa kufundishwa kidato cha tatu ama kuwepo katika mtihani wa kidato cha nne, cha sita au vyuoni.

Wapo wahafidhina watasema kuwa mada zisiporudiwa inamfanya mwanafunzi kusahau mapema hivyo itaonekana ni sawa na kazi bure, hembu tukubaliane jambo wale ndugu zetu wa afya wanaosoma miaka mitano ina maana na wao ule mwaka wa tano hawasahau kweli walivyofundishwa mwaka wa kwanza. Nao pia husahau ila bado mfumo huo huo ndiyo unaotumika mpaka kesho, ninachokiamini ni kuwa teknolojia imekuwa mno hivyo ni kitu rahisi kwa zama hizi kufanya Literature review kupitia hardcopy zinazopatikana maktaba au kupitia softcopy mitandaonii hivyo sioni kama ni sababu ya kusalia na huu mfumo wa kurudiarudia.

Wengine watasema kuwa kinachofundishwa shule ya msingi na sekondari hutofautiana lugha kwa hiyo ni vitu tofauti. Hapa napo inabidi patizamwe vizuri, kama imeshindikana Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia kwa ngazi zote za elimu hakuna ubaya kutumia Kingereza lakini isiwe sababu ya kurudiarudia mada na ikiwezekana madarasa ya chini yangetumika kufundishia lugha ya Kingereza pekee kabla ya kuanza kufundishana maswala ya zama za kale za binadamu. Yaani kama kunakuwa na mtihani aidha wa darasa la nne au la saba ama la sita kwa mfumo huu tarajiwa wa 7:4:2/3:3 basi mpaka mwanafunzi anaingia kufanya mtihani huo ajue vizuri lugha ya Kingereza kwa kusoma na kuandika aive kwenye grammer, tenses na vitu vingine kuhusu lugha hiyo ili kusudi anapoingia darasa la juu yake ajifunze moja kwa moja na kwa undani topic ya colonialism na siyo kuanza kufundishwa kwa juu juu mada ya vitangulizi vya ukoloni.

Endapo mawazo haya yatatiliwa mkazo itaturahisishia kukabiliana na maadui wa taifa hili vinginevyo tutaendelea kutembelea ringi. Mbali na hayo tunaweza pia kufikiria nje ya boksi namna nyingine tutakayoweza kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali tukiwa na umri mdogo. Wazazi wanatakiwa kutumia vizuri muda wa watoto wao kwa kuwapatia mafunzo ya ziada kwa mfano kuna miezi minne kwa mhitimu wa darasa la saba kabla hajajiunga na kidato cha kwanza hivyo basi badala ya kuhangaika na pre-form one wangewapeleka kwenye mafunzo ya ufundi kama vile VETA kwa ajili ya kupata ujuzi wa ziada. Ipo miezi mitatu baada ya mitihani ya kidato cha pili inatosha sana binti kujifunza charahani au kwa kijana kujifunza kuhusu biashara ya mitumba ama vijora pale kariakoo. Kuna miezi saba baada ya kidato cha nne pale zipo shughuli nyingi ambazo kijana wa umri chini ya miaka 18 anaweza kujifunza na kuzifanya. Yote kwa yote Mwenyezi Mungu aendelee kutuangaza na kutupa busara za kuyabeba haya na ukawa mwanga mbele ya maadui zetu haswa ujinga.
 
Upvote 7
ujinga ndiye adui kuu anayewapa nguvu wengine.
Na kama tungetambua kuwa ujinga ni kosa kubwa wakati upumbavu ni dhambi kabisa tutapiga hatua....... tusikie.

Inahitajika kuokoa muda unaotokana na kurudia kusoma mada ya aina moja ikiwezekana mfumo uliopo vyuoni wa kutoisoma tena mada uliyoifanyia mtihani baada ya kujifunza
Hili nnaunga mkono sana, tusirudierudie mambo tupate muda zaidi tujifunze mambo anuwai.

. Yote kwa yote Mwenyezi Mungu aendelee kutuangaza na kutupa busara za kuyabeba haya na ukawa mwanga mbele ya maadui zetu haswa ujinga
Adui ujinga ndiye aliyetoa kosababishi cha sie kuendelea kuteseka sababu ya ujinga yaaani daaaah
 
ninachokiamini ni kuwa teknolojia imekuwa mno hivyo ni kitu rahisi kwa zama hizi kufanya Literature review kupitia hardcopy zinazopatikana maktaba au kupitia softcopy mitandaonii hivyo sioni kama ni sababu ya kusalia na huu mfumo wa kurudiarudia.
Ukitaka kumnyima mali mwafrika mfichie kwenye kitabu. Ni msemo ambao sina uhakika kama kweli ndivyo unavyotamkwa ila hutumika sana mtaani namaanisha kuwa kitendo cha kuwashauri watanzania watumie mfumo utakaokuwa ukiwafanya warudi maktaba mara kwa mara ndiyo sababu ya kuwafanya wasiuelewe mfumo huo unaotutambulishia.

Achilia mbali hiyo teknolojia unayozungumzia maana watanzania wengi haswa hao wanaokimbizana vizuri na teknolojia wanajua zaidi website za ngono kuliko kuliko website za kujifunza mambo muhimu, ukikagua simu zetu whatsup tuna magroup mengi ya pono kuliko ya kujifunza yaani ukiona kuna group tofauti na la pono ujue ni la shule, familia au la kujifunza kitu kinachokuingizia kipato( mfano la kazini, kujifunza kupika keki au la kutangazia vitenge na vipodozi).
Yaani kama kunakuwa na mtihani aidha wa darasa la nne au la saba ama la sita kwa mfumo huu tarajiwa wa 7:4:2/3:3 basi mpaka mwanafunzi anaingia kufanya mtihani huo ajue vizuri lugha ya Kingereza kwa kusoma na kuandika aive kwenye grammer, tenses na vitu vingine kuhusu lugha hiyo ili kusudi anapoingia darasa la juu yake ajifunze moja kwa moja na kwa undani topic ya colonialism na siyo kuanza kufundishwa kwa juu juu mada ya vitangulizi vya ukoloni.
Mawazo yako still ni mazuri but Tanzanians we are so rigid, we are solid enough to accept abrupt changes so i dont think if these with D-nne will understand what you say.

Kifupi ni kama tumeridhika na maswala ya kupotezewa muda na mfumo huu wa elimu watakuona huna cha kuwashauri kwa kuwaambia wasome lugha tu kwa hiyo miaka minne mpaka sita ya shule ya msingi kutokana na kuamini katika mazoea yaani watakwambia "Tangu zamani tunasoma hivi wewe ni nani mpaka utubadilishe" ila siku Profesa kutoka ufaransa atakapoliona hilo na kuwaambia watakubaliana naye yaani hatujawahi kuaminiana kuwa tunaweza kuwaza kama wazungu.
 
Mawazo yako still ni mazuri but Tanzanians we are so rigid, we are solid enough to accept abrupt changes so i dont think if these with D-nne will understand what you say.
Kam cool braza mabadiliko ni mchakato hakuna anayeyapokea moja kwa moja bila pingamizi but its adaptation and through it(adaptation) we can made it(mabadiliko)
 
Back
Top Bottom