Kupitia shutuma za Marekani kwa Rwanda, Rais Kagame anatakiwa aachane na tabia ya kukiuka Mikataba kana kwamba hajasoma

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,651
Reaction score
1,129
Tabia mbaya kama hii ya raisi Kagame kugeuka makubaliano sana sana inafanywa na watu wasiokuwa na elimu lakini kwa msomi kama Kagame pamoja na cheo chake kuwa na tabia kama hii ya kukiuka makubaliano ya Mikataba ni tabia ya hovyo sana na anapaswa kuwa na aibu

Ifike mahali angalao basi viongozi waheshimu vyeo vyao vya uraisi

Cheo cha uraisi kuendeshwa kwa namna hii ni mambo ya hovyo na ya kuonewa aibu na kila mtu

Tunamkubali sana raisi Kagame lakini tafadhali asituaibishe tena tafadhali

Ikiwa raisi hajakubaliana na Mikataba basi anapaswa kuacha kutia sahihi badala ya kutia huku akiwa na manung'uniko
 
Nini tena jamani
 
Huu mjadala unaonyesha tabia ya baadhi ya watu kupenda simulizi rahisi kwa matatizo magumu.

Kumchora Rais Kagame kama mtu “anayekiuka mikataba kana kwamba hajasoma” ni kauli nyepesi kupita kiasi na inayopuuza uhalisia wa siasa za kikanda.


Marekani haina rekodi safi ya kuheshimu mikataba ya kimataifa, lakini inapotoa shutuma ghafla huonekana kama mlezi wa maadili.

Hilo ndilo tatizo. Rwanda haifanyi maamuzi yake kwenye vitabu vya sheria pekee, bali kwenye usalama wake wa taifa, hasa ikizingatiwa historia ya mauaji ya kimbari na vitisho vinavyotoka mashariki mwa DRC.



Kama mikataba ni takatifu, basi itekelezwe kwa wote, si kuitumika kama fimbo ya kisiasa dhidi ya nchi ndogo zisizo na sauti kubwa kimataifa.

Tatizo la Congo halikusababishwa na Kagame, wala halitatatuliwa kwa kumfanya yeye kuwa mbuzi wa kafara.

Hoja za juu juu na shutuma za upande mmoja hazileti amani, zinachochea unafiki wa kimataifa. Kinachohitajika ni ukweli mchungu, si propaganda laini...
 
Marekani inadai Kagame ndiye amekiuka makubaliano waliyowekeana na Congo lakini hakunyooshea kidole Congo
Walikuwa watatu katika Mkataba
Trump msimamizi
Congo na Rwanda
Pande hizi tatu zinadai Kagame ndiye amewageuka
Kwanini amegeuka wakati alikubali kutia sahihi?
Alipaswa akatae ikiwa alikuwa na shaka
Ndiyo sababu ya kutafsiri kitendo hiki kama makosa na hasa kwa raisi cheo kikubwa sana
 
Amekiuka makubaliano yapi?
 
Amekiuka makubaliano yapi?
Walikubaliana Rwanda iondoe Jeshi lake Congo lakini wanashangaa bado kuna Jeshi lake lipo Congo kwa siri sana
Wanashindwa kumwelewa kwanini anafanya hivyo wakati walishakubaliana
 
Kama amerika itapata chake katika mkataba huo uliokiukwa hawatamnyakua, ila kama atawabania wataruka naye, trump hana masihara kwa maslahi ya nchi yake
 
Kama amerika itapata chake katika mkataba huo uliokiukwa hawatamnyakua, ila kama atawabania wataruka naye, trump hana masihara kwa maslahi ya nchi yake
Ana kauli mbiu yake ya MAGA Make America Great Again
Kama ulivyosema hana masihara na hacheki na wowote sio 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…