Kupokea taarifa mbaya

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Habari gani waungwana..?

Kumekuwa na watu ambao wakipokea taarifa mbaya huwa wana panic na wengine kupelekea hata kufa so hili ni tatizo.
Kuna kupanic kwa kawaida ila kuna wengine duh! Wana zimia au kupata tatizo lolote kiafya sasa hapa badala ya kupunguza tatizo unaongeza tatizo!
Chukulia mtu uliyempelekea taarifa kwa bahati mbaya baada ya kumwambia tatizo anazimia alafu tatizo uliokuja kumwelezea yeye ndo anajua solution yake!
Nini kitatokea hapo kama sio tatizo juu ya tatizo..?

Binafsi ningependa kushauli hivi kwa kuwa taarifa mbaya unaweza kuipokea muda wowote weka wazo hili akilini mwako kwamba muda wowote unaweza kutokewa na jambo baya au kupokea taarifa mbaya.
hali hii inaweza kukusaidia kwani unakuwa tayari ushaweka wazo hilo kwenye akili hata yakikupata mshituko utakao kuwa nao sio mkubwa kivile.
hayo ni mawazo yangu sijui mdau mwenzangu wewe unasemaje juu ya hili..?

Karibuni....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…