Kuporomoka kwa SHILINGI Je kuna uhusiano na kufa kwa Mashirika ya kizalendo?

manizzle

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2015
Posts
3,421
Reaction score
4,320
Wachumi naomba mnijuze je kuna uhusiano wowote wa kuporomoka kwa thamani ya shilingi na kufa kwa mashirika yetu? Wakati viongozi na wananchi kwa ujumla tunajiuliza kwa nini SHILINGI yetu inaporomoka, tunatakiwa pia kujiuliza haya:
· Iko wapi UFI?
· Iko wapi TANGANYIKA PACKERS
· Iko wapi GENERAL TYRE?
· Iko wapi URAFIKI, SUNGURA-TEX, MWATEX, nk
· Iko wapi RTC?
· Iko wapi SUKITA?
· Iko wapi MMMT
· Iko wapi 'BENKI YA USHIRIKA NA MAENDELEO VIJIJINI' (sio hii CRDB ya sasa)
· Iko wapi UDA?
· Iko wapi KAMATA?
· Iko wapi RELI YA TANGA?
· Iko wapi NMC?
· Iko wapi ATC?
· Iko wapi Zana za Zilimo (ZZK) Mbeya?
· Iko wapi Retco?
· Iko wapi Tancati Almasi?
· Iko wapi Tumbaku Moro?
· Iko wapi Katani Tanga?
· Iko wapi Zabibu Dodoma?
· Iko wapi Nemco na TATEPA?
Unaweza ongezea orodha ya mashirika haya na pia kujua kama bado yako na kama yanafanya kazi. Hivi nini kilisababisha kufa kwa haya mashirika?
WAKO WAPI WALIOKUWA WAKURUGENZI NA MAMENEJA wa viwanda na mashirika hayo?

Tunaambiwa Tanzania ndo nchi ya pili kwa kuwa na mifugo mingi Africa, sawa.
Je soko letu la mazao yatokanayo na mifugo ni nchi zipi? na ni kwa kiasi gani sekta hiyo inatuingizia fedha za kigeni?

Tunajinasibu kuwa na utajiri wa dhahabu, almasi, chuma, TANZANITE, nk ambayo tayari yameshaanza kuchimbwa, bado Gas, mafuta, uranium, vimetuingizia fedha za kigeni kiasi gani?


Eti tuna vivutio vingi vya utalii, je kuna uwiano kweli kati ya wingi wa vivutio hivyo na kile tunachopata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…