Kuporomoka kwa shilingi, wafanyabiashara walia Kariakoo

Wengi walifiiri maendeleo ni kuwa na bidhaa za nje sasa mnalia nini? kazi kubwa ilofanyika kumlaumu mwalimu Nyerere imewafikiasha hapa sasa iweje watu mnaanza kulia lia wakati viwanda vinakufa mlisema bora vife vinatutia hasara. Wengine vibanafsishwe kumbe walonunua walitaka kukunua ardhi wakaua viwanda na kuuza vipuli nchi jirani.

Nchi hii tulikuwa na Tipper kiwanda cha kusafishia mafuta kabla ya Kenya, leo sisi tunasafisha mafuta nchi jirani. Tulikuwa na viwanda vya nguo leo China inapiga hatua kubwa kimaendeleo kwa mtaji wa viwanda vya nguo. Nyerere alituancha na viawanda sijui 7 vya Korosho leo viko wapi? halafu bado watu mnaichagua CCM kuongoza nchi, haya kesho sijui tunalazimika kuichagua UKAWA, ambayo hakuna Mtanzania hata mmoja anajua mwongozo wao katika ujenzi wa Uchumi. Tulipokuwa na Chadema tulijua wana lengo gani wana nia, nini msimamo wao juu ya uwekezaji nchini na kukuza viwanda.

Siko la kufa huwa halisikii dawa!
 
mbona una kichwa kigumu sana wewe. nimetolea mfano kama fenicha za ndani ambazo kiuhalisia ukienda pale manzese utapata nzuri tu. au unaweza kuweka hata oda. sasa huelewi nini hapo?
Serekali ndo inayo nunua fenicha kutoka nje.
 

subiri mwezi ijao! mafuta juuuuu! CCM has stolen our money! BVR ya Dola million 200 ya nini?
 
huu ndo muda muafaka wa kununua na kuuza bidhaa ndani. hii importation kila siku inachangia sana kutugarimu kama taifa.
yabaki yale ya lazima tu kama mafuta. ila tabia ya kuagiza mpaka fenicha za ndani malaysia au kule bondeni ikome kabisa.

Ndani nako kuna bidhaa zinazozalishwa na kiwanda kipi?Uwezo huo hatuna mpaka hapo tutakapoweza kufufua viwanda vyetu
 
kwani hiyo dola imepandishwa na wafanyabiashara wa kariakoo? kwani ni wafanyabiashara wa kariakoo tu ndo wanaoathirika?nilichosema ni kuwa impotation isiyoyalazima kama fenicha za ndani sijui dawa za meno/miswaki na kadhalika zikome. sijui ni kitu gani huelewi hapa.

 
nakubaliana na wewe kwa 85%. nayo iache pia. maana sasa hiyo ni anasa kwa uchumi tulionao.
kwahiyo unakili kuwa serekeli ndo inayo didimiza uchumi, badala ya kuhakikisha unanawiri
 
mbona una kichwa kigumu sana wewe. nimetolea mfano kama fenicha za ndani ambazo kiuhalisia ukienda pale manzese utapata nzuri tu. au unaweza kuweka hata oda. sasa huelewi nini hapo?

Tatizo mafundi seremala usanii mwingi. Na hawafikirii kujiupgrade
Sasa si bora niende kariakoo nikajinunulie mchina bila longolongo.
 

Kuna Daktari tena mkubwa sana katika nchi hii anaongoza Taasisi kubwa ya pesa. Anaitwa Dr. Kimeo alisema kuendelea kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ni faida kubwa sana kwa Watanzania.

Sasa nyinyi mnalalamika nini? Ina maana nyinyi mnajua sana kuliko huyo Dr. Kimeo?!
 
MA Tanzania hatuna akili nafikri tukae kimya tu dawa ituingie sawasawa maana najua kwa akili ugoro ya MA Tanzania Oktoba tena tunatoa kura kwa akili fupi iongoze akili ndefu = akili ndogo kutawala akili kubwa by Mch. Msigwa! Kikwe.the hakuwa na akili ya kuiongoza Tanzania wajinga wakubwa nyie! Na huwa nashangaa sana ninaposikia eti mburura naye kasoma uchumi! Hivi anazijua ABC za uchumi huyu? Sasa hivi Punda naye anataka urais jamaaaaaamani hebu tuwe waungwana!
 
Shilingi imesababisha mfumuko wa bei. Mshahara/kipato bado ni kilekile. Maisha yanazidi kudidimia na mbaya zaidi hakuna import substitute industries hata kwa basic goods kama malazi, vyakula na madawa.
To make things even worse vitu muhimu kama tuition fees na rent unatakiwa ulipe in $$ ama the equivalent!!!
Eeee Mungu tunusuru sisi waja wako
 
Bidhaa zipi? Kwa viwanda vipi? Maji ya uhai? Sabuni za ukwaju? Tuache usanii. Tumeua viwanda halafu tunatamba tununue bidhaa za ndani?

Tiles, toothpic, timber fanicha, bidhaa za chuma, gypsu, cemente, sukari, mchele, ngano, kahawa, maziwa, mafuta ya kula, nk
 
Tiles, toothpic, timber fanicha, bidhaa za chuma, gypsu, cemente, sukari, mchele, ngano, kahawa, maziwa, mafuta ya kula, nk

Kwa hiyo huwa mna import hata hivyo? Kweli ni aibu. Hebu jichunguze tena halafu urudi hapa kutoa comments
 
leo nilikuwa kariakoo kuna nguo huwa na nunua Tshs 20 leo nimekuta 28 wamegoma kupunguza
 
kwahiyo unakili kuwa serekeli ndo inayo didimiza uchumi, badala ya kuhakikisha unanawiri
rudi ukanisome post yangu ya kwanza utanielewa. maana kila kitu kiko huko. tatizo lenu mnarukia tu bila kujua mwanzo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…