wazazi;
Katika jamii nyingi za kileo, 'upofu' wa wazazi katika malezi unapelekea vijana kuamua kuishi kadri wazazi wao ama wanaowazunguka wanavyokubaliana nao. Kama mzazi anaona sawa bintiye kutoka na vivazi vya kudhalilisha, unadhani binti huyo atakubaliana na masharti ya mumewe kuhusu mavazi?
mfano; Kama binti/kijana haulizwi wala kudhibitiwa kwao uhusianio wake na mpenzi/wapenzi wake (wengi) katika umri wao mdogo, unadhani itakuwaje kesho/keshokutwa atapofumaniwa na mwenza wake na kesi hiyo kupelekwa kwa hao wazazi?
Sayansi, na teknolojia;
Pamoja na mazuri ya sayansi na teknolojia, zamani kulikuwa na restrictions nini kinachofaa kuangaliwa na watu wa umri gani au jamii gani. Mnaokumbuka enzi zile Drive inn Cinema, Avalon, Empress, Newchox, Empire, Tivoli na Sapna (morogoro), Metropole Arsuha... sinema zilikuwa classified na huingii kama umri haukuruhusu! Urahisi wa upatikanaji tekinolojia kwa njia ya simu, internet, umepelekea vijana wengiu kujifunza mambo ambayo hapo awali yalikuwa mwiko kujifunza achilia mbali kutaka kuyajua. Hata sinema za kibongo siku hizi aaaaaah, mambo nje nje!
Imani;
wengi tunazaliwa either wakristo/waislamu/baniani, au singasinga.
Ama kwa kukosa nafasi kutokana na msongo wa maisha au kukosa msisitizo toka kwa wazazi na jamii inayotuzunguka, Imekuwa ni nadra kusoma mafundisho ya vitabu na kufuata miongozo ya dini zetu jinsi ya kuishi kwa heri, heshima na taadhima. Kama una imani, na unaamini 'hukumu' basi utaogopa, na kujirudi. Kinyume na hapo, unakuta mtu anaponda mali tu kwa kudhani siku ya siku akishaungama yote yataisha,...usipoipata hiyo nafasi je? una miadi na 'minister of Justice' aliyepo mbinguni?
mila na desturi;
tunazijua mila na desturi zetu? au mila hukumbushwa pale binti anapotaka kuolewa tu kwenye utoaji wa mahari?
'Upofu' wa mila za kigeni;
Kwenye miaka ya sitini, serikali iliyapiga marufuku mashindano ya urembo (Ms Tanzania), ...wajanja (dada'ngu kina Farida fashion, Khadija mwanamboka, nk) wakatumia 'mianya' kuanzisha maonyesho ya urembo na mavazi mpaka serikali ilipoyaruhusu tena mashindano haya. Leo hii tuna Ms Utalii, Ms vyuo vikuu, Ms Universe, Ms Tanzania, Ms Redds, mpaka majuzi tumeshuhudia Ms 'Totoz'...
Kwa serikali kuachia wazi maeneo kunakopelekea mabinti wengi kuwa na muono mfupi wa maisha, yaani sex sells. No wonder, tunashuhudia mabinti kati ya miaka 16-23 kwa wingi sasa waporadhi watumike kama bidhaa (na bidhaa haichagui mnunuzi) badala ya ku pursue higher education, na maisha bora ya kifamilia.
...nitarudi na 'blah blah' nyingine...