Makanyagio
Senior Member
- Jun 25, 2009
- 125
- 30
Mm ni kijana umri ni zaidi ya miaka 30. nilipatwa na tatizo la mbegu kupungua kila baada muda fulani (meizi kazaa) na niliwahi kufanikiwa watoto uko nyuma lakini kwa sasa imekua mtihani, kwani kiwango cha mbegu kimekwenda chini sana. nimeshawaona watalaam mbalimbali wa mambo ya uzazi na kufanya vipimo mbalimbali, kwa mujibu wa madaktari mitambo ipo safi hata wao hawajui/hawaoni ni kwanini mbegu hazizalishwi inavyostahili. Wanasema kwa sasa ni tatizo kubwa kwa watu wengi na chanzo/sababu hakijafahamika. Nimetumia dawa mbalimbali nilizoandikiwa na maDr hao pamoja na kufuata masharti ya mavazi, chakula, unywaji nk. lakini bado sijafanikiwa.
Kwa yeyote anayefahamu dawa/mitishamba inayoweza kusaidia kuchochea kuongeza uzalisha wa mbegu atu/anijuze tafadhali. Naamini wapo wengi wenye tatizo kama hili hivyo kwa kuweka dawa hizo hapa na namna/mahali pa kuzipata utakuwa umesaidia wengi.
Nawasilisha.