Kupungua kwa damu

Watu pori

Senior Member
Joined
Jan 15, 2017
Posts
100
Reaction score
39
MTU kupungukiwa na damu mwilini unaweza ukatumia vyakula gani na ili kuweza kuirudisha kwenye kiwango chake ? Ama kunavidonge gani unaweza ukapewa na ikarudi sawa
 
Kula matembele kwa wingi ,kuna juice anaitwa lucela sijui,inasiaidia sana na kuna dawa unakunywa vijiko viwili kwa siku nayo nzuri kina nimesahau
 
MTU kupungukiwa na damu mwilini unaweza ukatumia vyakula gani na ili kuweza kuirudisha kwenye kiwango chake ? Ama kunavidonge gani unaweza ukapewa na ikarudi sawa
Kupungukiwa damu kuna sababu nyingi ambazo husababisha ni vyema ukazifahamu kwanza sababu zinazosababisha upungufu huo wa damu, mara nyingi upungufu wa damu mwilini husababishwa na kupungua madini chuma mwilini(iron) ambazo hizi hufanya kazi ya kubeba oxygen kutoka kwenye mapafu kuleta kwenye moyo na moyo kuisafirisha oxygen hiyo kwaajili ya shughuli za utengenezaji nguvu mwilini ATP molecules hivyo nilazima ujue chanzo chake kwanza ila baadhi ya vyakula vinavyoongeza damu kwa wingi na haraka zaidi ni
Maharage haya yanamadini chuma mengi sana
Dagaa pia
Mboga jamii ya majani mfano mchicha matembele n.k
Pia karoti na matunda kama nyanya n.k
 
Asante sana kwa kunipa somo
 
Maini na nyama nyekundu kama ya ng’ombe, mbuzi au kondoo, mchicha, broccoli, sukuma wiki na ule matunda kama machungwa au mananasi mara tu baada ya kula
Red meat na maini ina iron, matunda yana vitamin C ianaikamua iron vizuri wakati wa digestion
 
Kula matembele kwa wingi ,kuna juice anaitwa lucela sijui,inasiaidia sana na kuna dawa unakunywa vijiko viwili kwa siku nayo nzuri kina nimesahau
Tumia hemovit,sharubati ya rozela,sharubati ya mboga za majani,mboga za majani zenyewe au chemicola ila mboga hizo zichemshwe tu kiasi usiunge(weka chumvi tu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…