Kupungua uwezo wa tendo la ndoa

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,203
Reaction score
37,906
UGONJWA WA KISUKARI NA JINSI YA KUEPUKA

Kisukari ni ugonjwa ambao unasababishwa na kongosho kushindwa kuzalisha insulini au mwili kushindwa kutumia insulini ambayo inazalishwa ktk kongosho, Sukari (glucose) ikiingia ktk mwili kama ikizidi kongosho huzalisha glucgone homoni ambayo hutumika kubadilisha glucose kwenda kwenye glycogen ambayo inahifadhiwa kwenye misuli, kama mwili ukifikia kuwa hauna sukari ya kutosha glucagon huibadilisha glycogen kuwa glucose na kutumika ktkt mwili kwa hiyo kama kongosho ikishindwa kuzalisha glucagon hapa ndipo chanzo cha sukari ya kushuka huanza na mtu kuugua kisukari cha kushuka.Kwasababu cell za mwili huanza kushambuliwa.

AINA ZA KISUKARI.

Kuna aina mbili za kisukari.

1.KISUKARI CHA KURITHI.

Hichi ni kisukari ambacho mtu hurithi kutoka kwa wazazi wake pindi tu anapozaliwa, kisukari hichi kongosho halijitengenezei insulini ya kutosha.

2.AINA YA PILI NI KISUKARI AMBACHO SIO CHA KURITHI

Hiki ndio kisukari ambacho kinatusumbua wengi kwa sasa ktk familia zetu,jirani zetu na dunia kwa ujumla.kisukari hichi kinasemekekana hadi 2030 asilimia hamsini ya watu duniani watakuwa wanakufa na kisukari,hii husababishwa na ina ya maisha tunayoishi,vyakula vya kemikali tunavyokula na ukosefu wa kufanya mazoezi.

VINAVYOSABABISHA KISUKARI

1.Kongosho kutofanya kazi vizuri au kutofanya kazi kabisa

2.Kula vyakula vyenye sukari nyingi

3.Kutofanya mazoezi

4.Kurithi kutoka kwenye ukoo

5.Matatizo ya figo na presha ya kupanda

6.Uzito kupita kiasi

ATHARI ZA UGONJWA WA KISUKARI

1.Kupungua uwezo wa kuona

2.Kupungua nguvu za kiume

3.Presha ya kupanda

4.Kutopona vidonda haraka

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

1.Uchovu mara kwa mara

2.Kukojoa mara kwa mara

3.Kupungua uzito

4.Kuhisi kiumara kwa mara

5.Kupungua uwezo wa tendo la ndoa

6.Maumivu miguuni.

Watu wengi wamekuwa wakitibiwa kisukari kwa muda mrefu bila kupona kwasababu asilimia kubwa ya dawa ambazo wanatumia haziendi kutengeneza kongosho ambayo ndio yenye matatizo matokeo yake wanapewa dawa ya kwenda kwenye sukari iliyondani ya damu.HIvyo watu wengi wanaamini kuwa kisukari hakitibiki sio kweli,kisukari kinatibika na atu wanapona hata kama mtu kaugua miaka zaidi ya kumi.
 


Asante sana kwa elimu yako hii? Lakini swali lililobaki hapa, ni Je, ili kupata matibabu sahihi kwa mtu mwenye tatizo hilo, ni dawa gani sasa ambayo anafaa kutumia?
 
Umesema kisukari kinatibika..sasa toa muongozo wa tiba yenyewe

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…