Kupunguza BP bila Madawa

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Habari Doctor na JF wote.

Naomba kuuliza kama kuna aina ya vyakula ninavyoweza kula ili kupunguza Blood Pressure kwa haraka.

Nimetumia Dawa kwa kipindi cha miezi michache na BP imeshuka toka 176/116 hadi hivi karibuni 152/93 kiwango ambacho bado sijakipenda. Je mbali na mazoezi kuna aina ya vyakula naweza kula kupunguza Pressure kwa haraka zaidi?

Nawakilisha
 
punguza mavyakula yenye mafuta.km michemsho manyama ya kukaanga na mavyakula yoote yenye kiwango kikubwa cha mafuta

kunywa maji ya kutosha pamoja na matunda na mboga mboga
 
Kila chakula unacho kula hakikisha kuna Garlic

Ikiwezekana andaa gali na asali kila siku kabla ya kulala
 
Kuna mtu amenishauri kutumia Food Supplement kama trevo, kwenu wenye uzoefu mnasemaje kuhusu njia hii?
 
chukua majani ya mlonge den yaanike kivulini yakishakauka yasage kisha tengeneza uji kikombe kimoja changanya na ule unga kiasi cha kijiko kidogo cha chai kwa mda wa wiki 2 utasahau kabusa hio BP
 
Samahani mkuu haya majani ya mlonge den naweza kuyapata kuyanunua wapi? Ahsante
chukua majani ya mlonge den yaanike kivulini yakishakauka yasage kisha tengeneza uji kikombe kimoja changanya na ule unga kiasi cha kijiko kidogo cha chai kwa mda wa wiki 2 utasahau kabusa hio BP
 
Mkuu mimi nilikua na 180/90 but ile hali ilinitesa sana badae niliidharau nikabadili life style vyakula kupunguza pombe nimeacha na siuwazii tena dawa natumia mara moja moja sana nisikiapo hali inabadilika ila usipende kupima pima maana unajiongezea bp pia ww ishi normally tuu mkuu
 
Naomba kuuliza kama kuna aina ya vyakula ninavyoweza kula ili kupunguza Blood Pressure kwa haraka.

Nimetumia Dawa kwa kipindi cha miezi michache na BP imeshuka toka 176/116 hadi hivi karibuni 152/93 kiwango ambacho bado sijakipenda. Je mbali na mazoezi kuna aina ya vyakula naweza kula kupunguza Pressure kwa haraka zaidi?

Nawakilisha[/QUOTE]
kama una tatizo...ni vyema ukalifahamu tatizo kiundani, ukiifahamu presha vizuri itakusaidia sana kuidhibiti, kitu cha muhimu zaidi kabla ya kuanza kutumia dawa za kushusha presha huwa ni kujua chanzo cha presha? pia katika presha kuna matibabu yasiyohitaji dawa mfano kupunguza kiwango cha chumvi unachotumia, pia kudhibiti uzito wa mwili na kutumia matunda na mbogamboga kwa wingi ila cha muhimu kuzingatia ni kwamba kukaa na presha ikiwa juu muda mrefu huweza kuleta na madhara kwenye mwili baada ya miaka kadhaa, hivyo ni vyema ikadhibitiwa mapema
 
Jitahidi kupungua uzito wako kwa kiasi kikubwa, uwe kwe the most minimum BMI yako! Fanya maamuzi magumu utaona matokeo mazuri haraka !
 
Samahani mkuu haya majani ya mlonge den naweza kuyapata kuyanunua wapi? Ahsante
miti ya mlonge imetapakaa sana bt kwa hapa dar ni rahisi sana kuipata kigamboni maana ilipandwa kwa wingi sana miaka ya nyuma kuna jamaa aliahidi kuja nunua mbegu zake
 
vitu vikubwa vinavyochangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa pressure ni kupunguza uzito. ukipunguza kilo 10 unaweza punguza pressure ya juu SBP hadi 20mmhg. inamaana unaweza toka 176 hadi 156. kingine ni kula mafuta machache, mbogamboga na na matunda. ukikaza unaweza punguza 10mmhg. punguza chumvi na pombe. kama umefanya yote na hujafika lengo dawa haziepukiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…