Kupunguza idadi ya Maegesho Kariakoo ili kuongeza usalama wa Watu na mali zao

Kupunguza idadi ya Maegesho Kariakoo ili kuongeza usalama wa Watu na mali zao

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2019
Posts
222
Reaction score
202
Nimesoma hivi karibuni Ufaransa itapunguza maegesho 70,000 ya magari katika mji wa Paris,hii inatokana na sababu kuwa maegesho ya magari yanachukua takribani nusu ya eneo la mji wa Paris yakiwa na idadi ya asilimia 13% ya watu katika mji wa Paris.

Hapa Tanzania eneo la Kariakoo ambalo ni eneo muhimu kwa uchumi wa nchi linahitaji mkakati unaofanana na huu kwani eneo kubwa la Kariakoo linatumika kwa ajili ya maegesho ambayo ni usafiri wa watu wachache.Licha ya haya maegesho kuleta ajira na kipato kwa serikali athari zinazoweza kupatikana kwa uwepo wake ni kubwa ukilinganisha na faida zake.Athari za maegesho kariakoo ni kama zifuatazo:

Kwanza ni ajali zinazosababishwa na ufinyu wa eneo la kariakoo kutokana na uwepo wa maegesho mengi.Watu wanaopita maeneo ya kariakoo mara nyingi waendesha vifaa vya moto kwa mwendo kasi maeneo haya na kusababisha ajali kila kukicha.Ajali hizi husababisha vifo,majeraha na uharibifu wa mali pamoja na kusimamisha uzalishaji mali.

Pili,uharibifu wa mazingira kwa hewa zinazotokana na nishati ya mafuta na kelele zinazosababishwa na magari ni miongoni mwa sababu kubwa ianyodhofisha afya za watu.

Tatu,wakati wa dharura kama ya moto,au janga lingine lolote tunahitaji sehemu ya kukutania ili kuondokana na eneo lililopata janga.Uwepo wa maegesho mengi katikati ya jiji unaweza kungeza ukubwa wa tatizo,mfano moto unaweza kutapakaa eneo ubwa la mji kwa kuwepo na magari abayo yanaweza kuungua na kuchochea moto kutokana na nishati ya mafuta iliyopo kwenye magari hayo.

Faida kuu tatu zinazoweza kupatikana kwa kuondosha maegesho Kariakoo ni pamoja na kuongeza usalama wa eneo hili muhimu kwa uchumi wa Taifa,kuongeza mzunguko wa biashara na kupunguza uharibifu wa mazingira.

Ili kuimarisha usalama wa mali na wananchi ni vema tukaweka utaratibu wa kuimarisha usafiri wa umma na kupunguza idadi ya maegesho eneo la kariakoo kwa usalama wa nchi yetu.

Kuwepo maegesho machache maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu,magari ya mizigo na yale ya viongozi wa serikali.Serikali ihamasishe ujenzi wa maegesho ndani ya majengo kwa ajili ya biashara na ada za maegesho ziwe za bei nafuu.

Spidi ya magari idhibitiwe na kufika 30km/hr kwa kuwepo kwa vidhibiti mwendo katika mitaa yote ya kariakoo ili kuzuia ajali kwa magari yanayoingia na kutoka.
 
Kariakoo imeharibiwa kwa rushwa na wanasiasa nyumba zote za ghorofa zilitakiwa kuwa na parking lakini pamoja na hiyo sheria kuwapo bado maghorofa yalijengwa bila parking.
Magari ya serikali yasiruhusiwe kwani nao ni sehemu ya tatizo
 
Kariakoo ina maeneo gani ya parking? Sehemu kubwa ya Kariakoo imefunikwa na machinga Tu.
Magari yote yanayopaki Kariakoo yapo pembezoni mwa barabara Tu,eneo ambalo la wazi ambalo Magari yanapaki ni STENDI ya mwendokasi Tu...
 
Watu wengi wangependa kwenda Kariakoo kununua lakini ufinyu wa mji kutokana na parking kuwa ndogo unasababisha watu wengi kutokwenda.

SErikali pia inaweza kuwekeza yale maeneo korofi kama vile jangwani,kwa kutengeneza parking na kutumia njia zingine kufika katikati ya mji
 
Baada ya tukio la Lugalo, Kama lilivyo ripotiwa na Kigogo?
 
Kariakoo ina maeneo gani ya parking? Sehemu kubwa ya Kariakoo imefunikwa na machinga Tu.
Magari yote yanayopaki Kariakoo yapo pembezoni mwa barabara Tu,eneo ambalo la wazi ambalo Magari yanapaki ni STENDI ya mwendokasi Tu...
Kumbe pale Mwendokasi Gerezani kuna sehemu ya parking za private cars? Huwa nahangaika sana kutafuta parking pale Msimbazi Polisi kwa mateja wale nalipa 2000.
Gerezani unalipa shingap? Nafasi inatosha magari mengi, au ukienda mchana unakuta pamejaa
 
Kumbe pale Mwendokasi Gerezani kuna sehemu ya parking za private cars? Huwa nahangaika sana kutafuta parking pale Msimbazi Polisi kwa mateja wale nalipa 2000.
Gerezani unalipa shingap? Nafasi inatosha magari mengi, au ukienda mchana unakuta pamejaa
Gerezani napaki asubuh kilasiku kwasabb ukichelewa unakuta parking imejaa tena ukifika kuanzia saa 3 utakuta pamejaa...
Sikuhizi watu wanapaki hapo stand ya mwendokasi na bei yake ni tsh 2000 Kwa kutwa Ila TATIZO hakuna kivuli kama pale Gerezani
 
Back
Top Bottom