u hali gani mkuu, napenda kukujibu kuwa bahati mbaya hamna dawa ya kupunguza mafuta mwilii zaidi zaidi kwa dawa za kuharisha ambazo zinashtua mwili vilivyo na si salama kwa afya yako,
Njia pekee isaidiayo mwili kupunguza na kumaliza mafuta mwilini ni kutotumia vyakula vya wanga na sukari ambako kutapelekea mwili usihifadhi mafuta mwilini na baada ya muda mwilikuanza kutumia mafuta yaliopo kwaajili ya matumizi mengine za shughuli za kilasiku za mwili.
Na hii ndiyo njia sahihi ya watu kutumia katika kupunguza uzito ulozidi