Kupunguza tumbo

KAUMZA

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
699
Reaction score
237
Salaam..

Miaka mitatu iliyopita mke wangu alijifungua mtoto kwa njia ya kisu. Mara baada ya kujifungua, hakulifunga tumbo lake kama ilivyo ada ya wanawake wanapojifungua. Kitu kilichosababisha tumbo liwe kubwa as if ana ujauzito wa miezi mitano.

Nishaurini, afanyaje ili tumbo lake lirudi ktk hali ya kawaida?
 
Vipi anatumia vidonge/dawa za kuzuia ujauzito?. Nitajie urefu na kilo zake kwa sasa.
 
Mpaka atakapojifungua tena ndio anaweza kulirudisha kwa kulibana, ila kwa sasa haiwezekani (hiyo ni kwa mtazamo wangu)
 
mweeee
haya matumbo ya uzazi ni majanga jamani, hasa ya kisu as kufunga ni tabu na mazoezi pia ni tabu.

nami nasubiri maoni ya wajuzi...
 

kama unona noma chukuwa cho
bo kinge mwanangu achana nae.
 
Hapana. Hatumii hayo madawa. Ana urefu wa cm 164 na uzito wa Kg 72

Uzito wake kwa ujumla umemzidi, anatakiwa afanye mazoezi ya jumla ya kupunguza uzito wa mwili mzima ambayo hatimaye yatapunguza pia tumbo. Soma taratibu maelezo yote yaliyopo hapa ukiwa na swali zaidi unaweza kuniuliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…