Kupush hashtags mtandao wa x

Kupush hashtags mtandao wa x

Chance ndoto

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
4,363
Reaction score
10,265
Habari ndugu zangu, Nimejaribu kushinda sana twitter sasa X siku ya leo.

Huwa naona sana matangazo ya siasa au biashara.

Tukae haswa kwenye siasa. Baada ya kufatilia maongezi mengi, na kubadirishana mawazo kupitia comments.
Kwanza naona mtandaoni siku za sikuhizi wamejaa sana vijana wa makamo 20-28 au 29.

Hakuna kabisa undugu Mitandaoni vijana wengi kule ukicomment wanaamua wao wakuweke kwenye kundi la chama flani.

Wewe lumumba, unahamia thread nyingine wanakuja watu wanakuona wewe upo kwa bilikanazi. Yaani ni vulu vavala.

Sasa, issue kubwa ni hii, naona kuna swala kubwa la kupush hashtag wenyewe wanaiita. Unaweza shangaa watu zaidi ya 20 at once, wameshusha maelezo na picha ya kufanana, wanasifia mara kaupiga mwingi, mara treni.

Wengine utakuta wanapost labda anauza viwanja watu zaidi ya hamsini, kama copy na paste.

Zaidi kuna kundi lenyewe hulitoi kwenye mlengo wa chama.

Swali je! Ni kweli vijana haawa wanalipwa na hawa watu. Then inaweza kuwa fursa kwa vijana.

La mwisho unawezaje kujitoa kuona watanzania wakitweet vile kwenye feed yako.
 
Back
Top Bottom