kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Katika shule na vyuo vingi kitengo cha maadili kimekufa, wengi wamebaki na kitengo cha Weledi Wa Akili (Mental Intelligence).
Utaalamu pasipo maadili ni sawa na gari linalotembea usiku likiwa halina taa au gari moshi linalotembea likiwa halina breki.
Taaluma na maadili ni kama pande mbili za shilingi, huwezi kuzitenganisha.

Weledi wa akili unahusu kufahamu, kuchambua, kupambanua, kukumbuka, kufikiri na kujenga picha ya uhalisia wa vitu.
Haigusi tunu kuu za mtu kama upendo, haki, uwazi, kujiamini, ukweli, uadilifu, heshima, hekima, utashi, kujituma, uadilifu, busara.
Mambo haya yanapatikana kwenye kitengo muhimu sana cha weledi wa mtu kinachoitwa Maadili ya Weledi wa Kiroho (Spritual Intelligence Values). Kitengo hiki hakihusiani na dini wala imani ya mtu, kinahusu maadili ya mtu mbayo ndiyo yanayojenga ukamilifu wake.
Dini zinasaidia tu kujenga kitengo hiki kama ilivyo elimu nyingine.
Kwenye Weledi wa Maadili ndiko kunazaliwa vipaji vya utambuzi wa hisia za mwanadamu na tabia za mtu za ndani ya roho yake.
Udanganyifu, wizi, chuki, hekima na upendo vyote haviko kwenye akili ya mtu, vinapatika rohoni.
Hivyo, Maadili ya Weledi wa Kiroho hubeba tunu kama amani, busara, hekima, uwazi, uaminifu na heshima, kujituma, haki, hamasa ya kazi, uzalendo, utu, wema, uadilifu hata kujitambua na kujiamini ndiyo maadili kwenye kitengo cha weledi la kiroho.
Wanafunzi wanafundishwa tatu jumlisha tatu jibu ni sita halafu wanakabidhiwa vyeti wakapambane na dunia wakati silaha mahususi (maadili) hawajapewa.
Wanapewa mtihani wenye mafundisho manyonge baada ya hapo wazazi pamoja tunashangilia matokeo ya mtoto wetu ambayo kimsingi yana upungufu.
Katika vyuo vikuu, wanafunzi wanakazana kukariri na kukumbuka vipengele vingi vilivyo kwenye kitengo kimoja tu cha weledi wa akili, maeneo mengine yamesahaulika.
Kujua aina ya magonjwa hakuna thamani kubwa kama kujua kutenda haki, kujua Vasco Da Gama alifika lini Rasi ya Tumaini Jema hakuna manufaa kuliko kujenga upendo, usawa, uwajibikaji, haki, mshikamano na uzalendo.
Nimewahi kusema huko nyuma kuwa unamkuta daktari bingwa aliyebobea kupasua moyo wa binadamu anambaka mfanyakazi wake wa ndani. Unamkuta waziri mwenye shahada lukuki ana gushi malipo hewa ya posho zake.
Mbunge aliyesoma hadi chuo kikuu anatukana matusi hovyo bungeni, yote hii ni kutokana na kukosa tunu ya maadili.
Wanafunzi wanapikwa na kuandaliwa kuwa wataalamu katika maeneo mbalimbali lakini hawajengwi kuwa watu wa kujenga jamii yenye haki, uwazi, ukweli, uaminifu, amani, kujituma, kujitambua, uadilifu na heshima kwa binadamu wenzao. Tunatengeneza wezi ambao wanaitwa wataalamu.
Kuna baadhi ya nchi ambazo masuala ya dini yapo nyuma sana lakini wananchi wake hawawezi kuchelewa ofisini, kugushi risiti, kuhonga ili kupata huduma na hawawezi kuwanyima wanyonge haki zao.
Nakumbuka hata enzi za Mwalimu Nyerere eneo hili la Maadili ya Weledi wa Kiroho lilipewa kipaumbele. Ndiyo maana ilikuwa vigumu kukuta mkuu wa shule anasukumana na walimu kuingia darasani kufundisha.
Ndiyo maana ilikua vigumu sana kwa madaktari kwenda kazini wamelewa kama ilivyo sasa.
Ilikuwa vigumu sana kwa waziri kufanya ngono na sekretari wake, haikuwa rahisi mwalimu kufundisha uongo darasani, maadili ya rohoni kwa watu yalijengwa kikamilifu.
Tuliona mambo yalikuwa yakienda kwa kasi japo nchi ilikuwa bado changa, na wasomi walikuwa wachache. Leo licha ya wasomi kuwa wengi nchi haiendei, kila sekta ina matatizo lukuki.
Kinachosikitisha sana ni kwamba licha ya kupanua vyuo vikuu na kusomesha maelfu ya Watanzania vyuo vikuu, bado suluhu ya matatizo yetu tumebaki tunaagiza wataalamu nje ya nchi waliopikika kwenye maadili ya weledi wa kiroho.
Mtu mwenye maadili na weledi wa kiroho akisema anahitaji mifuko 200 ya saruji kujenga daraja, atajenga kwa mifuko 200, tofauti na wataalamu wetu akipewa mifuko 200 kwa ajili ya daraja yeye anatumia mifuko 70 mingine anaiba ndiyo maana madaraja yanaporomoka kila kukicha.
Cha kushangaza tunajifanya hatutambui hili na kuliona kama geni miongoni mwetu kwa kuwalaumu watoto wetu, huku wazazi na mifumo ya elimu yetu iliyofubaa inawaanda kuwa wavivu, waongo, wadanganyifu, walaghai, wasiojituma, wasiopenda kazi,wasioaminika na wenye kukosa utu wala haki. Wanaotamani maendeleo kwa njia za mkato bila kufanyakazi. Kwa mwendo huu nchi itasonga mbele?
Source: MCL