Elections 2010 Kura Katika Familia Yetu: Slaa 57%

Allien

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2008
Posts
5,546
Reaction score
1,861
Historia ya familia yetu: Baba na Mama > 65 Years
Last Born: 30 years
Dini: Mixture of Christian and Moslem
Makabila: Mchanganyiko wa Makabila mawili. In fact manne kama ukienda generation mbili nyuma (Mababu na Mabibi)
Itikadi: Baba na Mama walikuwa makada wa CCM. Miaka ya nyuma 2005 wote tulichagua CCM.

Mgawanyiko wa Kura:

1. Baba=CCM (Hapo nyuma enzi za Mrema aliwahi kuwa NCCR, then CUF sasa CCM lakini anaikubali CHADEMA. Anaishi kwake)
2. Mama=CHADEMA. Alikuwa home kwangu sasa kaondoka awahi alikojiandikisha ili kura yake isipotee. Anaishi kwake)
3. Mimi=CHADEMA Naishi na wife
4. Wife=CHADEMA anaishi nami
5. Sister 1=CCM anaishi kwake
6. Sister 2=CCM anaishi kwake
7. Sister 3=CHADEMA anaishi kwake.

Majumuisho:
CCM: 3 = 42.86%
CHADEMA: 4 = 57,14%

Je, utafiti wa kweli wa familia yako ukoje?

Naomba kuwakilisha
 
Haaa haaa sister 3 anadai yeye na mumewe ni CHADEMA. Mume wake sijamjumuisha hapo juu.
 

Hii safi sana! Hongera mkuu, hata safari ndefu huanza na hatua moja.utafiti - familia,ukoo,kabila, kijiji, kata,tarafa, wilaya,mkoa hadi taifa!

Sounds good.

Sisi kwetu wote ni chadema.
 
Hii safi sana! Hongera mkuu, hata safari ndefu huanza na hatua moja.utafiti - familia,ukoo,kabila, kijiji, kata,tarafa, wilaya,mkoa hadi taifa!

Sounds good.

Sisi kwetu wote ni chadema.

Du! Wote ukiwa una maana wazazi wenu, familia yako na ndugu uliozaliwa nao? Magwanyo wake ukoje kiidadi na je mnaishi katika nyumba moja?

Nia yangu ya kutoa background hapo juu ni kuonyesha kuwa sina influence katika maamuzi yao.
 
uh, sie hatujafanya utafiti huo lakini nimegundua kwamba kuna kura za slaa asilimia 90 kwenye yetu family
 
uh, sie hatujafanya utafiti huo lakini nimegundua kwamba kuna kura za slaa asilimia 90 kwenye yetu family

Msanii, unaweza kutake trouble utupatie background na breakdown ya idadi. Nia ni kuwa tu-ezxtend research yetu wenyewe lakini tu tuwe wa kweli. Itatusaidia pia kujua hali halisi bila kutegemea SYNOVET au REDET.

Hebu kila moja na utupatie breakdown halafu tutafanya majumuisho.
 
mimi naishi na madogo wawili na mshkaji wangu mmoja, jumla wanne na wote tumejiandikisha kupiga kura, watatu ubungo na mmoja mbeya. Sisi wote ni CHADEMA. So my family is 100% CHADEMA
 

Baba na Mama ni wastaafu wa E.A.C wanadai mafao yao sasa wote wamehamia CHADEMA.
Mke wangu ni Dr. pale Muhimbili nae ni CHADEMA
Watoto wetu watatu wako vyuo vikuu ingawa vote ni siri ya mtu lkn najua watampigia nani
Mdogo wangu ni m/kiti wa chadema(W)
SASA HAPO CHANGANYA NA ZAKWAKO
 
Kwanza kabla ya yote,

Sisi 2005, tuliwachagua upinzani katika ngazi ya ubunge na diwani, diwani ni wa chadema, Mbunge ni wa Chadema(wilbrod slaa - karatu) na kura za urais wengi katika familia tulimpa kikwete 2005. lakini sasa upepo umegeuka!

Sisi katika familia wenye kadi ya kupiga kura tuko watu 8, wanne wa kiume na wakike watatu pamoja na mama wa nne. wengine wameolewa wengine bado, hatukai pamoja ila huwa tunajumuika mara chache, niliwatembelea kujua maoni yao hata bila kuwashawishi. wote wanapiga chadema pamoja na waume/wake zao.

Kweli Slaa ana kura ya kutosha kwetu, naweza kusema ni 100%
 
NAONA VIGUMU KUTOA TAKWIMU ZA ASILIMIA 100% YA NDUGU ZANGU WOTE NA MAMA MZAZI NA FAMILIA ZA NDUGU ZANGU WOTE . UGUMU NI KWA SABABU MATARAJIO YANGU HAINGIII AKILINI MWANGU KUWA KUNA WATU WANAOWEZA KUWA NA SABABU ZA HALALI NA ZA HAKI ZA KUIPIGIA CCM KURA.

Ninajua wapo watakaoipigia lakini kwa sababu watu wanatumia uelewa wa kawaida haiingii akilini watu wadanganyike tena mwaka huu.
Kiongozi mmoja alisema. Mtu akija kwako kukukopa mara ya kwanza , ya pili na ya tatu bila kulipa hata mara moja akija ya nne unaweza kukopea bado? Ni mawili labda yeye atatumia busara aone aibu ya kurudi tena. Au akirudi tena basi ni wewe ukatae kuwa kwa kuwa hujaweza kurudisha mara mbili imani yangu imekwisha.
INABIDI UMKOPESHE AMBAYE HANA HISTORIA YA KUKURUSHA HATA KAMA ANAKOPA KWA MARA YA KWANZA.
Kwa kifupi nina mama mzazi kura yake ni kule inakotakiwa kuwa - Anayewapinga mafisadi na kuleta Matumaini
Ndugu zangu 6 na familia zao - Kwa yule mgombea anayekataa kukubali bajeti ya chai ya bilioni 30
Mimi na familia yangu na watoto wangu kura zetu nne ni kwa mwenye sifa ya kufanya utafiti wa kile anachokisema na asiyeogopa kufanya maamuzi magumu. wala kwetu sisi kura ya mwaka huu sio siri.
Huwezi kuifanya siri kwani msimamo wa mtu juu ya udhalimu au haki hauwi siri.
Utagundua kuwa kwa makusudi kabisa wala sijamtaja mtu tunayempa kura wala chama wala idadi kamili ya kura zetu.
Ninajaribu kuamini kuwa busara zetu zitaleta asilimia 100 za kura kwenye haki.
Hatuchagui marafiki wala dini tunachagua misimamo na maono ya taifa. Marafiki tutakuwa nao lakini kura ni kwa viongozi mashujaa na wenye uwezo.
 
Nampenda sana mwanzisha thread hii so nice mimi na mume wangu na watoto wetu watatu wote level ya chuo kikuu tulipigia CCM 2005 mwaka huu wote tumejiambia hatudanganyiki tutawapa chadema hata kama mbunge na diwani ni mazezeta tunajua Dr slaa atawachapa viboko wafanye kazi na kurejesha heshima ya nchi
 
familia yetu baba alikuwa ccm ila mwaka huu ameamua lkwa nia ya dhati kuhamia chadema pamoja na family members wote ni chadema mwanzo mwisho
 
Isee sisi familia nzima tumikubali chadema baada ya ujio wa Dr Slaa ni watu 15. Watu 6 tupo ubungo na 9 wako tabata.

Kwa hiyo 100% chadema.
 
Mwaka huu kazi ipo. Sisi kwetu ni 50% - 50% CCM:CHADEMA
 
familia yetu:
Baba: CCM( tangu hapo mwanzo ni CCM mzuri tu-anaishi kwake)
Mama: CHADEMA (alliipigia kura CCM 2005 na kuvaa t shirt za kikwete sana tu..lakini saiz hata kilemba tu hataki kukiona ndani!- anaishi na baba)
Mimi: CHADEMA (niliipigia kura CCM pia 2005 na kugombania tshirt za ccm mitaani-naishi kwangu na sijaoa)
Mdogo wangu: CHADEMA( hakupiga kura 2005, but saiz amefikisha umri wa kupiga kura na amejiandikisha tayari kwa kuipigia kura chadema 31 octbr)
wadogo wengine 3: hawa bado wapo shule ya msingi..wanaupenda sana ule wimbo wa chadema wa ..tuwamwage tuwamwage wee...tuwamwage ccm!! ila bado wadogo kuonyesha msimamo wao kwa sasa kwani hata kwenye mkutano wa ccm walienda kuwaona ze commedy na wa chadema walienda kumuona dr.slaa..niliwauliza wanafata nini kwenye kampeni wakanijibu hivyo! -wanaishi na wazazi!)

MCHANGANUO: CCM=1
CHADEMA = 3
SAWA NA CCM= 25% CHADEMA = 75%

hapa sijajumlisha na ndugu wa karibu sana tunaoishi nao karibu na nyumbani!!
 
Je, utafiti wa kweli wa familia yako ukoje?

Faza na maza CCM dam (kwa sababu ya "JK original = Julius Kambarage")

Lakini kwa CCM ya "JK feki = Jakaya Kikwete". Hali iko hivi:

Faza CCM lakini atapigia Chadema.
Maza CCM lakini atapigia Chadema.
Dogo haeleweki(hana kadi) lakini atapigia Chadema
Mimi sieleweki lakini SIDANGANYIKI. Kura yangu Chadema.
Sister haeleweki. Alishakula kiapo. Atapigia Chadema.
Mwanangu (ana mwaka mmoja na kitu hivi.). Nilishamwambia CCM ni adui yako namba moja. Akaitikia "Baba".

Chadema = (5/6)*100% = 83.33%
CCM = 0.00%
CUF = 0.00%

Naomba kutoa hoja.
 
Kwangu
mimi = chadema
wife =chadema
mabinti 4 = wote chadema
chadema 100%
CCM 0%
 
HAHAAAA...mi nlimbandikia dogo(ABT 1YR) label ya ccm kenye baby-chair yake wacha aanze kulia!!loh...nkatoa fasta!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…