Mimi: CHADEMA
Mke wangu: CHADEMA (nimemshawishi hivi karibuni, alikuwa CHAUSTA)
Mama mkwe: Haeleweki eleweki, ila naona anaitajataja TANU, namuweka CCM
House girl: Nimechimba mkwara na kumletea picha ya Slaa na Mnyika aanze kuzikariri. Hata napo naassume kura yake imeharibika.
Kwa hiyo:
CHADEMA:............. 50%
CCM: .................... 25%
Zilizoharibika ......... 25%
NB: Naendelea na juhudi kuiokoa kura ya HG, ila mama mkwe naogopa nitaanzaje!
HAHAAAA...mi nlimbandikia dogo(ABT 1YR) label ya ccm kenye baby-chair yake wacha aanze kulia!!loh...nkatoa fasta!!
Faza na maza CCM dam (kwa sababu ya "JK original = Julius Kambarage")
Lakini kwa CCM ya "JK feki = Jakaya Kikwete". Hali iko hivi:
Faza CCM lakini atapigia Chadema.
Maza CCM lakini atapigia Chadema.
Dogo haeleweki(hana kadi) lakini atapigia Chadema
Mimi sieleweki lakini SIDANGANYIKI. Kura yangu Chadema.
Sister haeleweki. Alishakula kiapo. Atapigia Chadema.
Mwanangu (ana mwaka mmoja na kitu hivi.). Nilishamwambia CCM ni adui yako namba moja. Akaitikia "Baba".
Chadema = (5/6)*100% = 83.33%
CCM = 0.00%
CUF = 0.00%
Naomba kutoa hoja.
Kwenye familia yetu
Dingi yeye piga ua ni CUF utadhani Mpemba
Mama yeye 2005 alimpigia Kikwete hadi leo bado ana tishet za Kikwete lakini ameahidi kumpigia Slaa
Mimi sidanganyiki 2010 hata ukiniamsha usiku namjua mtarajiwa wangu
My wife wangu yeye hata kadi yake ninaitunza mimi ni wa kumtuma tu kafanye hiki.
Mdogo wangu ninayemsomesha yeye anafuata ya kaka yake
Mama mdogo yeye ni mpambe wa mgombea ubunge wa chadema huyo hata mimi simfikii upenzi
Tatizo liko kwa dingi nina wasiwasi anaweza kumbadilisha mother.
Mchanganuo
CHM = 4
CUF = 1
Undecided = 1
Ila kinachonifurahisha familia yetu haina harufu ya CCM ndani.
ila kwa kifupi mi nawaomba chama tawala wasipuuze CHADEMA kwa kweli inaweza ikawashangaza.
Mbona Kikwete kamtuma mke wake kwa nini mimi nisimtume mke wangu usitake kutenganisha ndoa yangu ebo.hivi bado tuko kwenye ulimwengu huo? (hapo kwenye red)
Mbona Kikwete kamtuma mke wake kwa nini mimi nisimtume mke wangu usitake kutenganisha ndoa yangu ebo.
kwetu:
Babu na Bibi Upande wa Baba =CCM damu,
Bibi na Bibi upande wa mama = CCM
Baba = Kada wa CCM, lakini Snitch-ataipigia kura CHADEMA
Mama = CHADEMA DAMU,
Mimi = Sina Chama, kura yangu kwa CHADEMA
Mdogo wangu wa kiume = CHADEMA, ana card kabisa
Mdogo wangu wa kike = CHADEMA,
Mdogo wangu mwingine hajafikisha miaka 18, ila ni CHADEMA damu.
NB. Babu na Bibi wote walishafariki.
SO, KWETU CHADEMA 100%