Kura ya Katiba itatoa picha halisi ya Tanzania

Kura ya Katiba itatoa picha halisi ya Tanzania

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Naisubiri kwa hamu sana kura ya Katiba na ili nione Matokeo yake ambayo vyovyote vile itavyokua kwangu mimi itatoa picha ya nchi ya Tanzania kwa maana Viongozi wa Dini ya Kikristo wamewashawishi Waumini wao wapige kura ya HAPANA na Viongozi wa Kiislamu pia wamewashauri waumini wao wapige kura ya HAPANA!

Serikali inawataka wananchi wake waikubali Katiba na kupiga Kura ya NDIYO sasa huu ni Mtihani, Je Watanzania tanaheshimu zaidi Dola kuliko kitu kingine?

Kama Watz wakipigia kura ya ndiyo basi Dola itakuwa imeshinda na itathibitishia kile nilichokuwa nakiamini siku zote kwamba Watz Siasa siyo Mtu/watu bali ni Itikadi!

Na kwamba Watz ni watu makini sana na sio Wajinga kama wengi wanavyodhani, tunaweza kutenganisha Imani yetu ambacho ni kitu binafsi na Dola na sio kufwata watu au kikundi fulani cha watu yaani kwa maana nyingine tunaheshimu Dola na ni kitu kizuri sana huko mbele!

Long Live TanZania!
 
Kupiga kura ya HAPANA ni lazima ili kukwepesha madhara makubwa zaidi yatayoikumba nchi hii. Mapendekezo mengi ya wananchi yaliachwa na badala yake kubandikwa mambo ambayo hayana uhakika wa utekelezaji na mbaya zaidi katiba inalenga kumgandamiza zaidi Mtanzania kwa kumyima haki zake.
 
Kupiga kura ya HAPANA ni lazima ili kukwepesha madhara makubwa zaidi yatayoikumba nchi hii.

Mapendekezo mengi ya wananchi yaliachwa na badala yake kubandikwa mambo ambayo hayana uhakika wa utekelezaji na mbaya zaidi katiba inalenga kumgandamiza zaidi Mtanzania kwa kumyima haki zake.

Kwa taarifa yako sijatumwa na mtu yeyote. Kama unaweza kufuatilia posts zangu humu utaona (kama unaweza) kuona msimamo wangu kuhusu mustakabali wa nchi yetu.

Naona mmetumwa wengi humu jamvini kulinda maslahi ya mafisadi na mjue kwamba kwa hilo hamtafanikiwa kamwe. Watanzania wa leo si wa jana, na uamuzi wa kuipigia hapana katiba ya mafisadi ulifanyika kitambo sana...kwa kifupi tu ni kwamba mmechelewa!
 
Back
Top Bottom