Kura ya maoni katiba mpya, watu wa bara waje kwa pasport

Kura ya maoni katiba mpya, watu wa bara waje kwa pasport

semtema

Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
52
Reaction score
13
Jana nilishuhudia mkutano kati ya wananchi wa shehiya ya chukwani, wilaya ya makharibi Zanzibar wakitoa maoni yao kuhusu muundo wa katiba mpya. walihudhuria watu wa maeneo mengi hadi watu wabara waliohamia zamaani na vizazi vyao tokea 1910. kilichonishangaza ni pale mtu mmoja aliposema "watu wa bara wamezidi zanzibae, ukristo umezidi makanisa kibaoo kama uyoga wakati zamani yalikua matatu tu. sasa tunaomba watu wa Bara waje kwa visa na pasport wamezidi wanachukua nafasi zetu za kazi tu" me katika akili yangu nikajua tu kua huyu mwananchi hajawahi kusafiri wewe je unafkiri nini?:sleepy:
 
MAONI YA KATIBA HAYO!MIMI NAWAAMBIENI JAPO WATU WOTE WANA UHURU WAKUTOA MAONI NA DEMOKRASIA YA KUFANYA MAAMUZI;WATU HOTOFAUTIANA SANA KATIKA KUFIKIRI.KUNA WATU HUFIKIRI SANA NA WENGINE HUFIKIRI KIDOGO SANA.Nijambo la busara mno kama wale waliojaaliwa uwezo mkubwa zaidi watafikiri kwa niaba ya wenzao kwa kuwa wana upeo mkubwa zaidi.
 
loading.....................................error generated while trying to load the file
 
sawa sawa Zanzibar ni visiwa vidogo wakiachiliwa watu wakaingia kama ndani ya zizi la punda watavijaza na matokeo yake huduma zitakuwa hazifikii walengwa na mwisho visiwa vitazama.
 
@ semtema

anachokisema huyo mtu ni sawa hayo mambo zamani hayakuweko kule leo imekuwa ni kama dodoma au uchagani.
 
sawa sawa Zanzibar ni visiwa vidogo wakiachiliwa watu wakaingia kama ndani ya zizi la punda watavijaza na matokeo yake huduma zitakuwa hazifikii walengwa na mwisho visiwa vitazama.

Kuna udhibiti mwingine unafanywa kwenye mikoa mingine ya Tanzania au umeona Zanzibar tu ndio vulnerable? Itakuwa sasa tusema Lindi ni mkoa mdogo kwa hiyo watu wasiruhusiwe kuhamia huko au?
 
Back
Top Bottom