Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,275
WanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?

1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.


N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi

===============
 
Serikali 2 ndo mpango mzima! Tukiendekeza 3 Serikali ya Muungano itakuwa haina hata ardhi (ardhi si suala la Muungano) na itakuwa ombaomba kwa nchi washirika kwa kuwa haina vyanzo vya mapato vya kwake!
 
hakuna muafaka kwenye hili tusidanganyane. suluhisho ni wananchi wa pande 2 kupiga kura. Kwanza muungano wanautaka?

Hakuna kura ya maoni zaidi za kuipigia kura rasimu itakayopendekezwa na Bunge la Katiba! Wewe baada ya miaka 50 unaanza kujiuliza kuwa baba uliye naye ni baba yako au la, ya nini kujipa pressure ya bure? Huu Muungano ukivunjika Western Powers hazitakubali "another Somalia!" Waarabu na Al Shabaab/Al Qaeda nao hawatakubali kuona "Makafiri" wakikalia hivyo Visiwa! Don't think kwamba Tanganyika itakuwa salama eti kwa kuwa itakuwa si sehemu ya Zanzibar!
Think BIG brother/sister!
 
Serikali 3 is the best option kwa upande wangu.

Serikali mbili ni kuendeleza kero za muungano na pia katiba ya Zanzibar ya sasa ni tatizo kwa muundo uliopo.

Serikali moja itakuwa vigumu ku-manage kuiendesha.
 
Wazo zuri ila tatizo langu ni kuwa je ikitokea watu wa Zanzibar hawataki muungano hali watu wa Tanganyika wanataka Muungano, ili tatizo litatuliwaje?

Solution iko kwenye Ibara ya 98 ya Katiba ya JMT, 1977, yaani kupeleka Azimio Bungeni la Kuvunja Muungano! Lazima zipatikane kura theluthi 2 kila upande, otherwise Muungano is here to stay!
 

Ongeza mamba 4 kwa wasiotaka muungano.
 
Ninapenda muungano wa serikali moja.

Sababu ni kuwa kana nia ya mabadiliko ya katiba ya sasa ni kuondoa matatizo yanayalalamikiwa basi tujisahishe kwa kuwa na serikali moja na huu kwangu ndio muungano.

Kimsingi haya mawili chini ndio suluhu ya katiba yetu
(1) Serikali moja ya jamuhiri ya muungano wa Tanzania

au

(2) Serikari mbili yaani serikari ya Zanzibar na serikari ya Tanganyika, huku tukiwa na umoja wa Tanzania.

Mengine ya serikali 2 na 3 ni kubaguana hivyo hakuna haja ya kutumia dhana ya muukano bali ushirikiano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…