Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Baada ya kutembea karibu Tanzania nzima, nadiriki kusema ya kwamba wanaoshabikia kura ya maoni yoyote ile iwe katiba au sijui nini hawaishi nchi hii ya Tanzania!
Tuchukulie kwa mfano hii inayoitwa Katiba. Nilichokiona huko mikoani, wilayani na vijijini ni kwamba zaidi ya asilimia 85% ya wananchi hawawezi hata kuandika neno katiba na kulisoma achilia mbali hata kuelewa maana yake.
Sasa mnataka wapige kura ya ndiyo ama ya hapana kwa kigezo gani? Utapigaje kura kwa kitu usichokielewa, halafu mnaita Katiba ya Wananchi? Ni kwa nini hizo fedha msiwekeze kwenye elimu, maji safi na kutibu maradhi badala ya kupoteza kwenye kitu kisichoeleweka?
Kuna tofauti gani na wakoloni waliokuwa wanawekesha mababu zetu saini za dole gumba na kijimilikisha ardhi na maeneo makubwa?
Ama kweli tofauti ya Mkolononi na Mwafrika mweusi ni rangi tu!