Kura ya maoni, Ukawa wavutana Dar

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,536
Kitendo cha Chama cha Wananchi (CUF) kufanya uchaguzi wa Kura za Maoni katika majimbo ya Kawe na Ubungo yanayoshikiliwa na wabunge wa Chadema, kimeibua hisia tofauti miongoni mwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Mvutano huo unatokana na kinachoelezwa ni makubaliano ya vyama hivyo kuwa kila kimoja kiandae wagombea wake katika majimbo yote ambao watashindanishwa katika Ukawa, bila kuhusisha majimbo ambayo tayari yana shikiliwa na vyama vinavyounda umoja huo.

Mbali na kigezo hicho, mgawanyo wa majimbo unazingatia matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010, idadi ya madiwani kwa kila chama, matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014, mtandao wa chama nchini na nguvu ya mgombea iwapo Chadema kitamsimamisha katibu mkuu wake, Dk Willibrod Slaa kwa mara ya pili.

Juzi, CUF ilifanya uchaguzi wake wa kura za maoni katika Mkoa wa ya Dar es Salaam ambapo pamoja na majimbo mengine, iliwapitisha Leila Hussen kukiwakilisha chama hicho katika Jimbo la Kawe na Mashaka Ngole katika Jimbo la Ubungo.

Mvutano wenyewe
Kutokana na hatua hiyo, vyama vya NCCR-Mageuzi na NLD vimesema CUF imeanza kwenda kinyume na makubaliano ya Ukawa, ingawa CUF na Chadema wameeleza kuwa haikuwa kosa kufanya kura ya maoni kwenye majimbo hayo.

Ingawa viongozi hao wametofautiana kimtazamo kuhusu hatua hiyo ya CUF, wamesisitiza kuwa kuweka mgombea mmoja wa upinzani kupitia Ukawa bado ni njia sahihi na pekee itakayowezesha kuiondoa CCM.

Kauli ya NLD

Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alisema Ukawa haijafikia uamuzi wa kuiachia Chadema majimbo ya Ubungo na Kawe, lakini CUF imekosea kuwasimamisha wagombea katika majimbo hayo kwa kuwa vikao vya kuwapata wagombea wa upinzani bado vinaendelea.

"Ukweli ni kwamba hakuna kikao cha Ukawa kilichopitisha kuyaacha majimbo hayo kwa Chadema, ila CUF wamefanya kosa moja tu, kutangaza wagombea wake hadharani. Kama ni mchakato wa maandalizi, walipaswa kuwaanda wagombea hao ndani ya chama chao ili kusubiri uamuzi wa vikao vya Ukawa," alisema Dk Makaidi na kuendelea;
"Hata sisi NLD tuna wagombea wetu Dar es Salaam, lakini hatuwezi kuwatangaza kwa sababu tunasubiri vikao vya Ukawa."

Alipoulizwa kuna tatizo gani kumtangaza mgombea sasa huku wakiendelea kusubiri vikao vya Ukawa alijibu, "Huku ni kuwachanganya wananchi. Kama kila chama kitatangaza mgombea wake sasa halafu Ukawa ikaja na mgombea mmoja, huku ni kuchanganya watu."


Wafuasi wa chama cha wananchi (CUF) wakimdhibiti kada mwezao aliyedaiwa kufanya vurugu wakati wa uchaguzi wa kura za maoni Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi
 
nilisma na ninarudia tena kusema...........NINA MASHAKA NA UMOJA WA UKAWA,
pigeni mawe.
 
Hao wawili wa mgongoni na yule anayefuatia, wanadhitije? Mbona kama wanamfanyia kitu cha kumsababishia maumivu makali sana? Wanamfanyaje?

Njia sahihi ilikuwa ni kumtoa nje ya kikao badala ya kumjeruhi kisirisiri. Kutofautiana siyo kugombana.
 

Kwani UKAWA ni chama??? Waacheni CUF wafanye maendeleo ya chama chao, mbona chadema wameshayakiuka makubaliano kitambo sana, hata mikutanoni wako bize wanamtangaza hadharani Slaa kuwa ndiye mgombea urais wa chadema, kwani hapo mliwashirikisha CUF katika uamuzi huo? Shida ya chadema ni kuua upinzani ili wakipata madaraka kusiwe na cha chochote chenye nguvu. Cuf wamewashtukia mapema.
 
Dah!Pilipili ya shamba niko mjini!Mh!!!!!!!!!!!lakini bado inawasha Mama yangu wewe
 
Hao wachumia tumbo ndoa yao bado changa,nilisema UKAWA sio chama ni Buguruni team afu watu wakajifanya kupinga sasa ona wasipopasuana mwaka huu sijui!!! ndoa yenyewe imezaliwa kutokana na kitendo cha kususa nikasema wakitupatia ufumbuzi kwenye yale majimbo 12 wanayovutana ya [COLOR=rgba(0, 0, 0, 0.701961)]1. Segerea 2 Temeke 3 Ukonga 4 Ilala 5Ilala 6.Kinondoni 7.Kigamboni 8. Serengeti 9.Mafia 10.Morogoro mjini 11.Kilosa 12.Mtwara mjini [/COLOR] wao ni vidume afu wakaruka kiunzi cha mgombea urais 2015 njia nyeupe Ikulu zaidi ya hapo wanafanya mazoezi ya kucheza kidukuView attachment 253537View attachment 253538View attachment 253539
 
Hizi ni changamoto za kawaida tuu ndani ya UKAWA .ccm mnafurahia ya UKAWA wakati kwenu hali ndo mbaya zaidi kuliko UKAWA.
 


Sasa nyie mna hofu gani na UKAWA kama mnajiamini .
 
Hawa hakika wamekula sumu ya panya wakijua haiui hawa sio bure inaelekea na wewe ni mmoja wapo nenda kaoloe hiyo ndoa yao bado changa sana teh te h teh hawa jamaa ni shidaa njaa mbaya!!

Naona pilipili ilo shamba imekuwasha kila mahali.............Mbaya zaidi sijui uliila nyingi maana hata choo chako kinaonyesha...............

Kawaulieze wenzako CAG kawapa ya aina gani MBUZI au KICHAA...........Naona UKAWA wamewatandika mpaka na ----- mwaka huu mnao.................

VOTE FOR UKAWA
 
mbona unahangaika na Umoja wa UKAWA ambao una mashaka nao waache wafanye yao .

Buguruni team,njaa mbaya wakifika Ubungo watapasuana kule vunjo fasta walimpata mgombea bado majimbo 12 lazima pachimbike!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…