Kura ya maoni ungependa nani awe mwenyekiti wa bunge la katiba?

Kura ya maoni ungependa nani awe mwenyekiti wa bunge la katiba?

Centrehalf

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2013
Posts
509
Reaction score
145
Salaam wana jamvi,

Kumekuwa na tetesi kuwa waziri wa Afrika Mashariki na spika wa zamani wa bunge la katiba mh. Samwel Sitta ni miongoni mwa wanaotaka kugombea uwenyekiti wa kudumu pamoja na mh. Andrew Chenge mwenyekiti wa kamati uchumi na mwanasheria mkuu wa zamani katika serikali ya awamu ya tatu nae ametajwa kuutaka uwenyekiti wa bunge la katiba.

Je wewe ungependa nani awe mwenyekiti wa bunge la katiba?

Nawasilisha.
 
kati ya mzee six na chege bora six' lakini mtu kama mahalu alifaa zaidi
 
Hivi hakuna mwengine anayegombea?........hao wawili wote hawafai
 
Kwanza bunge lenyewe limeshaniboa, huku kuahirisha vikao implication yake ni nini? Na hizi siku wanazokaa dodoma bure inakuwaje tukizingatia economic and political implications?
 
Ndg wanajf inasikitisha kuona mvurugano unaoendelea ndani ya bunge la katiba kabla hata ya kuanza kuijadili rasimu ya katiba mpya. Bunge hilo linaonekana pasuakichwa na wagombea uenyekiti wa bunge la katiba kutokana na chama cha siasa tena mmoja wao akiwa fisadi papa la kutupwa. Kupatikana kwa katiba mpya itakayokidhi haki na matakwa ya wananchi bado ni kiini macho.
 
Nani tena huyo?? Sisi tuna habari za Sitta kuchuana na Migiro!!! Sasa papa hapa ni nani kati ya hawa wawili?
 
Tuletee anayetoka chama cha mpira basi make unataka kujenga hoja ambayo haina mashiko kabisa kwa bunge hili.
 
Tuletee anayetoka chama cha mpira basi make unataka kujenga hoja ambayo haina mashiko kabisa kwa bunge hili.
Acha kutoa povu basi kwani umeshikwa pabaya? Inaonekana umelelewa kwa gharama za buku 7 kutoka Lumumba ndio maana unatoa povu kupita kiasi.
 
Chenge na Migiro ni mapandikizi ya mafisadi, ijapokuwa Sitta ni mnafiki wakati mwingine lakini bora huyo kuliko mijizi mingine
 
Halafu Migiri kadri siku zinvyosogea anajipambanua zaidi kuvinjari na kuwa kambi za mafisadi sijui ni kwa nini?, yeye hajioni lakini umma unamuona hiovyo, ni mara nyiongi anakuwa katika kundi lenye maslahi ya kifisadi badala ya upande mwingine. Kama ni njaa hana kihivyo, kama ni tamaa ya madsaraka ameshakamata ya kimataifa , hivi motive yake ni nini hasa?
 
Ninamaanisha Migiro
 
Hivi kati ya wale watu woote waliokusanyika dodoma wagombea wanaofaa ni hao tu kweli?
 
sina uhakika sana ila nadhani six kwa kiasi fulani anastahili
 
Back
Top Bottom