Uchaguzi 2020 Kura yangu 2020

Uchaguzi 2020 Kura yangu 2020

MICHAEL SON

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2020
Posts
458
Reaction score
536
Asalam,, Corona itapita . na uchaguzi utafanyika Inshaalah. iwe mwaka huu ama mwaka wowote ule, Allah akinilinda na kunipa uhai huu ndo utakua mustakabali ya kura yangu.

SITOMPA KURA YANGU MAGUFULI ,.
Niweke wazi kabisa siwezi kumpa kura yangu MAGUFULI japo nina kadi active ya CCM. kwa SABABU zangu binafsi zifatazo
1. KUONGEZA MAKATO YA BODI
YA MKOPO KUTOKAA 8%-15% KINYUME NA MKATABA Hili ongezeko limeniathiri sana ki uchumi kwani zaidi ya 50,000/= imekua ikikatwa kila mwezi katika MSHAHARA wangu wa mkia wa mbuzi uliokaa dormant Miaka 4 na sasa wa 5..

2. KUNIPIKONYA MSHAHARA WANGU WA DARAJA JIPYA 2015.
Wakati Mh JK Ana ondoka nilipanda daraja na July mwaka 2015 nikaanza KUPATA MSHAHARA mpya ulionipa nguvu na hali ya kutenda kazi hapa ni BAADA ya kutumikia cheo cha awali kwa Miaka 5, Ila BAADA ya huyu Rais MAGUFULI kuingia bila huruma alisitisha MSHAHARA wangu mpya niliopokea kwa miezi 5 tu,,, akaondoa stahiki yangu zaidi ya 200,000/=,,na hapo hapo kuniongezea makato kwa 7% nikawa na matumaini uhakiki ukiisha haki yangu itarejeshwa hadi leo nipo napuyanga na maisha,hakuna jipya ni Story zile zile

3. UGUMU WA KUFANYA BIASHARA .
Tangu huyu bwana apewe nchi kumekua na vikwazo lukuki vya biashara makadilio ya kodi makubwa,,na kulazimishwa kununu EFD mashine ilihali mtaji wangu hauzid hata 1M. pia mzunguko wa fedha umekua mgumu hakuna pesa hakuna wateja nikafunga biashara

4.KUDHULUMIWA FEDHA ZANGU ZA KOROSHO
Sikuchoka kupambana nikajichanga pamoja na kuomba MKOPO bank ,,nikakodi shamba la KOROSHO kwa mkulima mmoja huku lindi vijijini mavuno hayakua haba ,,nikauza nikitegemea 3300/= sh kwa kilo kama alivyo ipamba itanifuta machozi matokeo yake nikambiwa mm ni mlanguzi wa Kangomba sikulipwa zaid ya 6M.

Najua mara nyingi mnaiba kura ,,ila hata ukiiba Jua kabisa kura yangu sitokupa..
Niwaombe watanzania wenzangu mliopatwa na maswahibu kama yangu kwa namna moja ama nyingine unganeni na mimi Kajiandikisheni kama muda ungalipo,,na tukapiga kura ,,,,,,, WHAT A WORSE PRESIDENT EVER..( spare me some gramatical error)
 
Unaweza kua na mikosi yako huko kwenye maisha itokanayo na ukoo wako we unalaumu Rais tu

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
MIKOSI yangu imefanya Watumishi wote wasipate annual increment kwa Miaka 4?. who am I na ukoo wangu?.. MIKOSI YANGU Ndo imefanya wanufaika wote wa bodi ya mikopo kuongezewa makato?.. oooh who am I?

MIKOSI yangu Ndo imefanya wananchi wa mikoa ya kusini wanalia hadi leo NYUMBA nyingi zimechorwa na mabenki who am I na ukoo wangu?... use your brain ,,weeds isukupereke putaa Mkuu
 
Kura yako ni haki yako huku pia ikiwa ni silaha yako dhidi ya wanasiasa waongo, matapeli na mafisadi ambao hutoa ahadi nyingi za uongo, lakini usitegemee uchaguzi huru na wa haki kutoka kwa majambazi wa CCM.
 
Mimi kura yangu nimeshampa Dr Magufuli!! Hata usemeje hatudanganyiki!! Mzalendo huwezi kulalamikia kodi!
 
.
IMG_20200430_115849.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tz ninchi bora na tajiri zaidi East Afrika ukichkua KE,UG & TZ lkn nionavyo mimi!!
- Elimu tunashika mki
- Afya tunazidiwa.
- viwanda tunazidiwa.
- ukubwa wa majiji tunazidiwa.
- umeme tukoduni mpaka Ug wanatuuzia.
- maji na umwagiliaji tukoduni.
- furaha ya maisha tukochini.
- michezo tukochini.
- maelewano kimataifa wamwisho
- biashara tukochini.
Vitu tufanyavyo tukaongoza kwa nijuavyo,
- kwasasa koona.
- kuchati mitandaoni na kura.
- kuogopa mabadiliko yavyama.
- vyama duni vya wafanyakazi.
- mahakama na taasisi nyingi kuingiliwa.
- walimu wenyeuwezo duni
- kujisifu na kuendekeza siaza za vyama.
- mishahara duni
- .....
Kivipi nisichague mabadiliko? Bora hata kumpa uongozi shoe shiner kama Brazil mradi tusizoeane vibaya maujinga yanayofanyika yawekwe wazi na hatua zichukuliwe juu yao wanaotufelisha
 
Kijana umeongea kwa machungu sana. Mimi nilikuwa nshakataa tamaa na sikwenda kuboresha taarifa zangu kwenye daftari la kupigia kura. Ila kwa hili andiko lake nitafanya kila namna niboreshe na kura nipige.

Nilimpa kura 2015 ila kwa Sasa hafai hata sekunde kubaki Ikulu

Sent using Jamii Forums mobile app
keep that spirit burning ni nchi yetu sote
 
Tz ninchi bora na tajiri zaidi East Afrika ukichkua KE,UG & TZ lkn nionavyo mimi!!
- Elimu tunashika mki
- Afya tunazidiwa.
- viwanda tunazidiwa.
- ukubwa wa majiji tunazidiwa.
- umeme tukoduni mpaka Ug wanatuuzia.
- maji na umwagiliaji tukoduni.
- furaha ya maisha tukochini.
- michezo tukochini.
- maelewano kimataifa wamwisho
- biashara tukochini.
Vitu tufanyavyo tukaongoza kwa nijuavyo,
- kwasasa koona.
- kuchati mitandaoni na kura.
- kuogopa mabadiliko yavyama.
- vyama duni vya wafanyakazi.
- mahakama na taasisi nyingi kuingiliwa.
- walimu wenyeuwezo duni
- kujisifu na kuendekeza siaza za vyama.
- mishahara duni
- .....
Kivipi nisichague mabadiliko? Bora hata kumpa uongozi shue shiner kama Brazil mradi tusizoeane vibaya maujinga yanayofanyika yawekwe wazi na hatua zichukuliwe juu yao wanaotufelisha
kura yangu silaha yangu
 
Mbona kipindi cha kampeni bado sana?? Acheni uchochezi huu mara moja. Kura ni siri ya mtu
Ndo nimeanza na sitoacha Mkuu,,, najua wazi kura yangu ina nguvu ila haitoshi hivyo ntakushawishi na wewe na wengine,,,, NCHI YETU SOTE,,na huu ujinga mloleta awamu ya tano mkipewa hoja Zikawagusa hamjibu kwa hoja mnakimbilia kutushutumu kwa uchochezi? sasa wacha niongeze kuni
 
Back
Top Bottom