Elections 2010 Kura yangu siri yangu yako je?

Elections 2010 Kura yangu siri yangu yako je?

Shishye

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2009
Posts
269
Reaction score
1
Kura yangu ni siri isipokuwa kwa mgombea mmoja tu..... hili liko wazi wala sio siri tena.
1. Silali usingizi wa kutosha maana lazima nidamke usiku usiku kutokana na foleni.
2. Nikiugua sina matumaini ya kupona maana huduma za afya ni duni kuliko mfano
3. Elimu ya watoto wangu ni shida shule za kata!
4. Maji ni ya taabu, nanunua kwa madumu bila hata uhakika wa usafi wake
5. Ufisadi ndio nyumbani kwake, mwenye nafasi bila kufanya hivyo unaonekana zezeta
6. Uwajibikaji sifuri... kazi mtu hufanya kwa kuangalia maslahi (kidogodogo)
7. Kodi hutozwa kubwa, matumizi yake marufuku kuuliza. safari kwa sana, semina, magari ya kifahari kwa waheshimiwa, nk.
 
Kura yangu sio siri - ni Chadema tu. (Rais, Mbunge, Diwani)

Ukimpigia CCM huipigii maendeleo ya nchi unapigia maendeleo ya BMW (Baba, Mama na Watoto) a.k.a JK family
 
Back
Top Bottom