Mwafrika,
Mkuu hakuna sababu ya kulalamika kwani members JF ni zaidi ya elfu 22 na waliopiga kura ni watu elfu 8 tu. Hivyo kama kura za JK zinaongezeka ina maana Dr.Slaa anazembea sehemu fulani kuwavuta zaidi wananchi ambao kwetu sisi swala kubwa ni UCHUMI, lakini hadi sasa vyama vingi vinazungumzia zaidi Huduma za wananchi (Social services) baada ya kupewa madaraka... Hivyo yawezekana kabisa kwamba Dr.Slaa anakosea mahala hasa anapokuwa akijihami na kejeli za CCM badala ya kuendeleza somo la Utawala bora na kukuza uchumi wetu, vitu ambavyo ndivyo udhaifu mkubwa wa JK na chama CCM...
Ni wakati wa Dr.Slaa kuznugmzia Uchumi na kuendeleza vita juu ya Ufisadi na jinsi unavyoharibu maendeleo na pato la Taifa. Na kikubwa zaidi azungumzie policy zake ambazo zitaongeza Ufanisi ktk sekta zote za uzalishaji hasa akigusia AJIRA..
Tukumbuke tu kwamba Wapiga kura nchini ni watu waliozidi Umri wa miaka 18 ambao hawana kazi, elimu wala sifa za kupata ajira ktk sekta kubwa ya services inayokuwa haraka. Hawa ni maskini na hawawezi kusubiri wala kufikiria zaidi elimu ya watoto wao wenyewe hali maiisha yao ni duni hapo walipo. Hivyo hawapati hotuba ya kuwahakikishia ajira na maisha bora..
Taifa limekwama ktk tope, maisha yao pia yamesimama hviyo haijalishi ukiwapa ahadi za baadaye ikiwa leo hii hawaoni tumaini la kutoka hapo walipo..Kwanza, tutaweza vipi kutoka hapa tulipokwama na uhakika wa safari ambayo itawahakikishia ajira.