Kura za wajumbe wa Katiba Mpya wanaoogopa zisipotee

Kura za wajumbe wa Katiba Mpya wanaoogopa zisipotee

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569
Suala la kura ya wazi au ya siri limesumbua mjadala wa kanuni za bunge la katiba mpya:
Mapungufu: Kamati ya Prof Mahalu imelirudisha suala hili kwa wajumbe bila kulichambua (kulitafuna) na kulishauri
bunge. Hawakulitafuna vizuri, wamelirudisha likiwa bado gumu.
Mazuri: Mwenyekiti wa muda, Mh Kificho,hakufanya papara kulitolea uamuzi. Angekuwa mwingine angeweza tu kuwataka wajumbe wapige kura: wanaotaka kura ya siri na wanaotaka kura ya wazi. Yeye akaamua kwenda kulitafuna
mwenyewe kwanza kabla ya kulileta tena kwa wajumbe kwa uamuzi.
Ushauri: 1. Kwa baadhi ya vipengele vya rasimu ya katiba ambavyo ni nyeti kama kile cha serikali 2 au 3 ambavyo vyama vya siasa na vikundi vingine vilishatolea misimamo; wapo baadhi ya wajumbe ambao wamesema bayana kuwa
wataogopa kwenda kinyume na misimamo ya vikundi vyao baada ya mjadala kama maamuzi yatafanyika kwa
njia ya wazi. Vipengele visivyo nyeti hakuna tatizo kupigiwa kura ya wazi.
2. Huu ndiyo ukweli wenyewe. Hivyo mijadala mizito ya hoja itakayofanyika kwenye vipengele hivyo, hata iwe ya ushawishi gani haitakuwa na maana yo yote kwa wajumbe hawa kama maamuzi yatafanyika kwa kura za wazi.
Mtu anayeogopa huwezi ukamshawishi kirahisi tu kwamba asiogope utamlinda, yaani akararuliwe na simba
halafu ndiyo aje kupata ulinzi? Hivyo tutapoteza kura zao, kitu ambacho si kizuri hata kama ni chache.
3. Halafu fikiria kwa mfano, Waziri Mkuu (Mh Pinda) baada ya kusikiliza hoja nzito kuhusu serikali tatu
akashawishika binafsi kuunga mkono hoja ya serikali tatu. Akipiga kura ya wazi, wafuasi wake wengi
watafuata kubadili msimamo wao wa awali. Hivyo hivyo kama Mh Mbowe akapigia kura ya kuunga mkono
serikali mbili wafuasi wake wengi watamfuata. Na Mh Lipumba hivyo hivyo.
4. Ikumbukwe Bunge maalum la katiba lina wajumbe na siyo wabunge. Kuna tofauti kubwa kati ya mbunge
na mjumbe. Kazi ya mjumbe ni kuwasilisha tu kile alichotumwa (mwasilishi wa kundi lake) wakati mbunge
ni mwakilishi wa aliyemtuma. Mbunge ana power of attoney wakati mjumbe hana hiyo power. Sheria ya
mabadiliko ya katiba ilisema Bunge maalum litakuwa na wajumbe, si wabunge.

Tuendelee kumsaidia Mh Kificho kulitafuna suala hili kabla hajalifikisha tena kwa wajumbe kwa uamuzi.
 
Back
Top Bottom