na hiki ndicho kinachofata. ni ngumu sana mke na mamkwe wakae pamoja na waende sawa. mm na waifu tumepanga mbali na hom sasa kuna wkt waifu akaanza kung'ang'ana akakae na maza. nikawa nampotezea tu maana nawajua wote vizuri wawili. sasa alipokomaa nikamruhusu aende akakae mwezi mmoja. alikaa wiki kadhaa tu akarudi na complaints zilikuwa kibao. icho kipindi chote yupo kule na maza ilikuwa napokea simu za malalamiko kutoka kwa wote wawili. sasa ivi ni zaidi ya miaka 7 sijamsikia tena waifu aongelee mambo ya kwenda kwa mkwewe.Rudi nyumbani ila jipange kwa vita kati ya mkeo na mama yako
Hilo nenoTafuta kiwanja cha bei Chee Jenga atakama ni kaslope.
Tafadhari.
Usirudishe mpira kwa kipa.
Zingatia utakuja kishukuru au labda kama huna mpango wa kujenga familia.
Mke mtumie kama chanzo cha kupunguta ugumu mpe biasharaHabari wana JF.
Mie ni kijana nimeona na nina watoto wawili. Kimaisha sipo vibaya sana nashukuru Mungu. Changamoto kubwa inayonipa hardtime ni Kodi ninazolipa kwa ujumla kuanzia kwenye biashara mpaka nyumba ya kupanga ninayoishi,najiona nimekua na mzigo mkubwa wa kulipa kodi mpaka nashindwa fanya moves nyingine.
Nimewaza kitu ambacho sijui nitafikiriwa vipi na wanaonizunguka ila kwa upande wangu naona itakua ni ahueni!!
Nimewaza kuhama nilipopanga na nirudi nyumbani kwetu,kupunguza kodi moja na kuongeza nguvu kwenye biashara ili ni make at least na mie nijenge mji wangu,maana umri wazidi kimbia.
Naombeni ushauri wenu kama ninalowaza ni sahihi au si sahihi!!
Familia hana haja ya kuikimbia kama ni mtoto mmoja au wawili alafu wadogoo..! bora airudishe familia nyumbani ila yeye asiende kuishi hapo japo matumizi yatamkaba maana itabdi ajihudumie na ahudumie familia pia.Kimbia familia,upange kachumba ka elfu 20,
Utawatafutaga mambo yakiwa sawa
Kama bondi ya mama na mke haipo vizurii si uache mke upeleke watoto wako kwa mama mzee huna nyumba huna gari maisha yamekupiga bado unakomaa kuling'ang'ania janamke ambalo halielewani na mamako. Piga chinii peleka watoto kwa mama utachopata unakula na mama soon tu unajenga. Yani kwa maelezoo hayoo ni wazi huyo mwanamke ni mbinafsii na ndio anakurudisha nyuma kimaendeleo. Piga chini kama huna chochote unawaza nini wakati hakuna ata kugawa mali hapoNyumbani ni yupo mama na mdogo wangu tu.mzee alishatangulia mbele za haki.
Kiukweli bond ya mke na familia yangu si nzuri sana
Ila mpaka nimewaza hivyo nimeumia sana maji naona yapo shingoni.
Ila asante kwa ushauri wako mkuu
Mama mdogo wako..mke wako..watoto na wewe hiyo ni familia tayari so jipime kama utaweza kutoa mahitaji ukwepe kodi au ndo utabadilisha matumizi ya hela tu toka kodi mpaka matumizi plus ugomvi wa mama na mke maana hiyo ni lazimaaa uwepoo tu.Nyumbani ni yupo mama na mdogo wangu tu.mzee alishatangulia mbele za haki.
Kiukweli bond ya mke na familia yangu si nzuri sana
Ila mpaka nimewaza hivyo nimeumia sana maji naona yapo shingoni.
Ila asante kwa ushauri wako mkuu
Go East go West home is the best
Gentleman,
hongera kwa tathimini makini yenye maono na malengo ya mbali sana kwa siku zijazo, ambayo ni very positive kwa mustakabali na ustawi mwema wa familia yako.
Nyumbani ni nyumbani my friends, ladies and gentlemen,
fedheha za nyumbani hazina karaa ukilinganisha na za kwenye nyumba ya kupanga. Fedheha za nyumbani ni nzuri sana ukizigeuza positively na kua fursa ya kukufanya ufanye bidii zaidi katika kutafuta ili hatimae ujenge na kuhamia kwako kwenye amani na utulivu zaidi, lakini pia ukiwa na uhakika hakuna wa kukufukuza kwenu hata muwe mmebanana vipi.
Naunga mkono uamuzi wako wa maana sana, wa kujiformat upya na hatimae kujipanga vizuri na kujizatiti kuyafikia malengo yako walau ukiwa mahali salama 🐒
Sikubaliani na ushahuri wako huu.Kimbia familia,upange kachumba ka elfu 20,
Utawatafutaga mambo yakiwa sawa
relax gentleman,Mawazo kama haya mazuri uwe unayatoa pia kwenye hoja zako za kisiasa.
Kumbe unakuwaga na mawazo mazuri nilikuwa najuwa wewe ni mtu wa hovyo sana kwenye kila nyanja