Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 346
- 522
Copy & paste from Christian Bwaya from X social media!.
Mwanamume unaamini mwanamke akisoma anakuwa tatizo kwenye mahusiano, ‘hatawaliki’ na ataishia kuwa msimbe. Kwa nini sasa unasomesha watoto wa kike? Unawaandaa kuachika? Haya. Umeoa asiyesoma. Unamtawala kifikra kama unavyotaka. Lakini mbona yakijitokeza matatizo, unasema tatizo ni uelewa wake mdogo, kukosa exposure, na hivyo unapata shida sana kuendana naye kiufahamu.
Bado hujagundua tatizo ni udhaifu wa mwanaume? Kizazi cha wanaume dhaifu hupambana na mafanikio ya wanawake —matokeo ni kizazi cha wanawake wasio na imani na ‘uanaume’ wao.Kizazi hiki kikiukabili udhaifu wake, kikajifunza uongozi, kikajifunza kusimama kwenye nafasi yake, huzalisha wanawake wasio na haja ya ‘kushindana’ nao.Wanaume wa kizazi hiki tuna kazi kubwa ya kupambana na insecurities zinazotuaminisha kuwa matatizo yetu yanatokana na kujitambua kwa wanawake.
Tukijitambua tukapambana na unyonge unaotutafuna chini kwa chini hatutaogopa wanawake wenye mafanikio.