Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Vijana 131 kati ya vijana 3,698 waliokuwa kwenye mafunzo ya awali ya askari polisi kwenye shule ya polisi Tanzania zamani ikiitwa CCP ,wameshindwa kuendelea na masomo baada ya kufukuzwa shuleni hapo kutokana na makosa mbalimbali ikiwamo ya utovu wa nidhamu.
Hayo yamo kwenye Taarifa ya mkuu wa shule hiyo Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa polisi(SACP),Ramadhan Mungi wakati wa kufunga mafunzo ya awali kwa askari wapya wa polisi wa kozi namba moja 2023/2024.
Alisema oktoba mwaka jana chuo hicho kiliwapokea wanafunzi 3,698 na kati ya hao wanawake ni 1,997 na wanaume ni 2,601 ambao walianza masomo yaliyogawanywa kwenye vipindi vinne vyenye wiki 12 kila kipindi .
Amesema mafunzo yaliyotolewa kwa vijana hao ni pamoja na misingi imara ya kuwa askari imara ,mafunzo ya matumizi ya silaha,mafunzo ya kuwaongezea utimamu wa mwili na akili.
Mafunzo mengine ni pamoja na kupewa maarifa na ujuzi wa kazi za msingi za askari wa polisi ,kazi za msingi za kazi za polisi na utawala,sheria za msingi za polisi na haki za binadamu .
Mengine ni sheria za msingi za makosa ya jinai,sheria za msingi za mwenendo wa mashitaka ya makosa ya jinai.
Kuruta hao pia walipewa mafunzo ya ujuzi wa mawasiliano na matumizi ya teknolojia ya habari.
Awamu ya tatu ya mafunzo hayo yalihusisha kuwapa maarifa na ujuzi unaowezesha kutenda kazi zao za polisi ambako masomo saba yalifundishwa.
Masomo hayo ni pamoja na sheria ya ushahidi ,upelelezi,intelijensia,jinsi ya kushughulika na masuala ya usalama barabarani .
Masomo mengine ni afya ya jamii na ulinzi wa mazingira,jinsia na ulinzi wa mtoto,mafunzo ya ugaidi na imani kali,kudhibiti ghasia na kushughulika na majanga .
Kwa mujibu wa Kamishna Mungi,baada ya mafunzo hayo kuruta hao walipelekwa ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ambako walifanya kazi zinazofanywa na askari mwenye cheo cha konstebo ikiwamo kushika doria,chumba cha mashitaka ,kulinda wafungwa mahakamani,usalama barabarani.
Kazi zingine ni kusindikiza wafungwa,kusaidia waendesha mashitaka pamoja na dawati la jinsia .
Amesema vijana hao walihimisha mafunzo yao huko West Kilimanjaro ambako walipata mafunzo ya medali za mbinu za kivita.
Vijana hao walipimwa kiwango cha maarifa ,kiwango cha ujuzi katika kila somo na uwezo wa kutenda kwa vitendo .
Vijana hao pia walipimwa tabia kama zinafanana au zinaendana na tabia za askari polisi.
Soma Pia: Askari wanne wafukuzwa kazi kwa kufuta picha za kwenye kamera ya mwendokasi
Amesema mitihani ilifanyika kwa nadhalia na vitendo ambapo matokeo ya mitihani hiyo yakawasukuma nje vijana hao na kubaki vijana 3,567.
Mwisho